KILIMANI: PAA LA JUMBA NAMBA 5 LAANGUKA, WAKAZI WAHOFIA USALAMA WAO
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
KILIMANI: PAA LA JUMBA NAMBA 5 LAANGUKA, WAKAZI WAHOFIA USALAMA WAO
4 739 просмотров · 2 дня назад
ASAM Online TV
22,5 тыс. подписчиков
4 739 просмотров · 2 дня назад
Wakazi wa eneo la Kilimani, Mkoa wa Mjini Magharibi, wameingiwa na hofu baada ya paa la Jumba Namba 5 kuanguka, tukio lililoibua wasiwasi kuhusu usalama wa majumba hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mhe. Moh’d Ali Abdallah, amefika eneo la tukio kujionea hali halisi na kubaini mazingira ya tukio hilo.
Amesema Serikali inaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha usalama wao unalindwa, huku akiwataka wakazi kuchukua tahadhari ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Kwa upande wao, baadhi ya wakazi wameeleza namna tukio hilo lilivyotokea na kuiomba Serikali kuingilia kati kwa kufanya ukarabati wa majumba hayo ili kuimarisha usalama wao.
#Kilimani #Zanzibar #UsalamaWaMakazi #AsamOnlineTV #ZanzibarNews