MAREKEBISHO YA MISHAHARA ZANZIBAR YAFIKIA ASILIMIA 95
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
MAREKEBISHO YA MISHAHARA ZANZIBAR YAFIKIA ASILIMIA 95
2 666 просмотров · 23 ч назад
ASAM Online TV
22,5 тыс. подписчиков
2 666 просмотров · 23 ч назад
Maafisa Utumishi Zanzibar wametakiwa kuelewa vyema mfumo na miundo ya utumishi pamoja na utaratibu uliotumika katika marekebisho ya mishahara mipya, ili kuhakikisha taarifa za watumishi zinasimamiwa kwa usahihi.
Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Omar Haji Gora, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii, Maruhubi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Miundo na Maslahi ya Watumishi, Maulid Shaib Ahmad, amesema mafunzo hayo yameandaliwa kabla ya kuanza kwa malipo ili kuwawezesha Maafisa Utumishi kutoa ufafanuzi sahihi kuhusu stahiki za watumishi kwa kuzingatia elimu na uzoefu wao.
Aidha, imeelezwa kuwa marekebisho ya mishahara yamefikia asilimia 95. Watumishi watakaokumbana na changamoto wametakiwa kuwasiliana na Maafisa Utumishi au Wakurugenzi wao ili matatizo hayo yaweze kutatuliwa kwa haraka.
#MishaharaZanzibar #UtumishiWaUmma #Zanzibar #AsamOnlineTV #ZanzibarNews