Перейти к содержимому

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA JUMAPILI - IBADA YA KWANZA | 09 AUGUST 2026

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH

0:00 / 0:00

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA JUMAPILI - IBADA YA KWANZA | 09 AUGUST 2026

11 348 просмотров · Трансляция закончилась 1 месяц назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
64,5 тыс. подписчиков
11 348 просмотров · Трансляция закончилась 1 месяц назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA JUMAPILI - IBADA YA KWANZA | 09 AUGUST 2026 UJUMBE WA LEO: HAKI HULETA AMANI NA USTAWI Walawi 19 : 30 - 37 30 Zishikeni Sabato zangu, mpaheshimu patakatifu pangu; mimi ndimi Bwana. 31 Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 32 Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi Bwana. 33 Na mgeni akikaa pamoja nawe katika nchi yako, usimdhulumu. 34 Mgeni akaaye pamoja nawe atakuwa kama mzalia kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 35 Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo. 36 Mizani ya haki, vipimo vya haki, efa ya haki, hini ya haki, ndivyo mtakavyokuwa navyo. Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri. 37 Zishikeni sheria zangu, na hukumu zangu, na kuzitenda. Mimi ndimi Bwana. A. Maana ya Haki 1. Ni kitu anachostahili mtu ama anachopaswa kuwa nacho (Rights/Entitlements) Mfano; kuishi, kumiliki mali, kutoa maoni, kupata elimu, n.k ii. Ni usawa na kutopendelea (Justice/Fairness) Hii hutokana hasa na masuala ya sheria, tamaduni na desturi. Haki hii huitwa hukumu; ni kuamua mambo kwa usawa na ukweli iii.Ni ukweli, Usahihi na Maadili mema (Truth/Righteousness) Haki hii ni kutenda mambo kwa kufuata misingi ya wema na kuepuka dhuluma na uovu. B. Maana ya Amani i. Ni hali ya utulivu (Amani ya moyo - tranquility), ukimya mshikamano/utengamano/maelewano ii. Ni hali ya kutokuwepo ukandamizaji, hali ya vita na machafuko iii. Ni hali ya uwepo wa uhuru wa mawazo na fikra na maamuzi (demokrasia) C. Maana ya Ustawi 1. Ni mandeleo ya kifikra, kiroho na kiuchumi ii. Ni hali ya kuzaa na kuongezeka Matunda ya Haki kwa mujibu wa Somo. Matunda ya Haki kwa mujibu wa Somo; 1. Haki ni nuru kwenye jamii (Mathayo 5:14-16 & Waefeso 5:9) Waefeso 5:9 9 kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; 2. Kumtendea mtu haki ni kujitendea haki wewe mwenyewe Luka 6:37-38 37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. 38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa. 3. Amani ni zaidi ya utulivu wa kawaida, ni tunda la Haki (Isaya 32:17) 17 Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. Pamoja na hayo na uzuri wa haki, kwa dunia ya sasa ukizungumzia haki huenda ukawa unajiweka hatarini, huenda ukachukiwa na baadhi ya watu hii ni kwa sababu huruma ya mtu mwovu ni ukatili (Mithali 13:10) 10 Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana. "Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili." Lakini sisi kama kanisa NI LAZIMA TUSEME JUU YA HAKI kwa sababu "Kweli imechipuka katika nchi, Haki imechungulia kutoka mbinguni." (Zaburi 85:11) Kwanini watu wasiotenda haki hawapendi haki? 11 Kweli imechipuka katika nchi, Haki imechungulia kutoka mbinguni. 1. Kiburi kama matokeo ya "poor personal character" 2. Kusahau ulikotoka (Somo la Walawi) 3. Tabia ya shetani ya kupinga haki ya Mungu (Mungu ni Mungu wa haki lakini shetani ni kinyume chake - "Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele." (Yohana 10:10) 10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. HITIMISHO: Sisi ni nuru ya ulimwengu na haki ni nuru. Matunda ya haki ni Amani na Ustawi. Mhubiri: Mwinjilisti Benson Mmari. Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com