Перейти к содержимому

WANANCHI 327 WAFIKIWA NA KAMBI YA KIBINGWA YA MOYO MBEYA

MbeyaYetuOnlineTV

0:00 / 0:00

WANANCHI 327 WAFIKIWA NA KAMBI YA KIBINGWA YA MOYO MBEYA

55 просмотров · 3 недели назад
MbeyaYetuOnlineTV
254 тыс. подписчиков
55 просмотров · 3 недели назад
MBEYA: Wananchi 327 wamefikiwa na huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kupitia kambi maalumu ya kibingwa ya siku tatu iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya. Kati yao, wananchi 73 walibainika kuwa na changamoto za moyo, ambapo walipatiwa ushauri wa kitaalamu na baadhi kupewa rufaa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi. Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Dkt. Fredrick Mlowe, ameipongeza Serikali na wataalamu wa afya kwa kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi. Mratibu wa kambi hiyo, Joyce Komba, amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kugundua mapema magonjwa ya moyo na kuchukua hatua stahiki. Kambi hiyo imefanyika katika kuadhimisha Siku ya Moyo Duniani, yenye kauli mbiu: “Usipuuze mapigo ya moyo: Zingatia Kinga, Uchunguzi wa Mapema na Maisha yenye Afya.”