DC. ITUNDA AFUNGUA MAONESHO YA KITF 2026 KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA MBEYA
MbeyaYetuOnlineTV
0:00 / 0:00
DC. ITUNDA AFUNGUA MAONESHO YA KITF 2026 KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA MBEYA
97 просмотров · 6 дн. назад
MbeyaYetuOnlineTV
254 тыс. подписчиков
97 просмотров · 6 дн. назад
MBEYA: Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mheshimiwa Solomon Itunda, amefungua rasmi Maonesho ya Biashara na Uwekezaji Nyanda za Juu Kusini (KITF 2026), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, yaliyofanyika katika Kata ya Itezi, Jimbo la Uyole, mkoani Mbeya.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, Itunda amewahimiza wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kuonyesha bidhaa na huduma zao, akieleza kuwa maonesho hayo ni fursa muhimu ya kutangaza biashara, kupanua masoko na kutumia fursa zilizopo katika sekta ya biashara na uwekezaji.
Amesema maonesho hayo yanalenga kuwaunganisha wafanyabiashara na wateja pamoja na wadau mbalimbali wa biashara, huku yakiwapa nafasi ya kutangaza bidhaa na huduma zao na kujenga mahusiano yatakayosaidia kukuza shughuli zao za kiuchumi.
Kwa upande wake, Mratibu Msaidizi wa Maonesho ya Biashara na Uwekezaji Nyanda za Juu Kusini, George Mwaitenda, amesema KITF 2026 yanalenga kuonyesha shughuli mbalimbali za kibiashara, kutangaza bidhaa na huduma zinazozalishwa na wafanyabiashara, pamoja na kuibua fursa mpya za biashara na uwekezaji.
Mwaitenda amesema maonesho hayo pia yanatarajiwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa kutoa nafasi kwa wafanyabiashara, wawekezaji na wadau wengine kukutana, kubadilishana uzoefu na kutafuta fursa za ushirikiano.