Перейти к содержимому

OTHMAN AAGIZA MIONGOZO YA MATUMIZI YA ARDHI ZILIZOINGIA MAJI YA BAHARI

ZANZIBAR YETU

0:00 / 0:00

OTHMAN AAGIZA MIONGOZO YA MATUMIZI YA ARDHI ZILIZOINGIA MAJI YA BAHARI

4 003 просмотра · 16 ч назад
ZANZIBAR YETU
10,8 тыс. подписчиков
4 003 просмотра · 16 ч назад
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, ametoa maelekezo kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) ikishirikiana na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, kukaa pamoja na kuweka miongozo na sera ya pamoja ya matumizi bora ya ardhi zilizoingia maji ya bahari pamoja na utunzaji wa mazingira. Amesema bila kuwepo kwa miongozo thabiti ya serikali, kila muwekezaji anaweza kutumia maeneo hayo kwa namna anavyotaka yeye mwenyewe. Othman ameyasema hayo leo, Novemba 02, 2026, kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na viongozi pamoja na wananchi katika ziara ya kukagua shughuli zinazosimamiwa na taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Aidha, alisisitiza kuwa usimamizi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja ili kuifanya jamii na dunia kuwa sehemu salama ya kuishi. "Serikali inapaswa kutengeneza sera bora na rafiki za kuwawezesha wananchi kusimamia mazingira na kujenga urafiki na taasisi za serikali, badala ya kuzikwepa kwa hofu," alisema Mhe. Othman. Wakati huo huo, Othman amewashukuru wadau binafsi wa mazingira kwa namna wanavyoisaidia Serikali katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira, pamoja na kutengeneza fursa za ajira kwa wananchi. "Takataka hizi za plastiki, vigae, mabaki ya vyakula na majani, kwa wingi huu kama zingekuwa uraiani zingeenda kuleta milipuko ya maradhi. Hata hivyo, kupitia ninyi mmeweza kuzichakata na kuzifanya bidhaa zinazotumika tena, huku mkizalisha ajira kwa vijana wetu, kiukweli mumezifanya changamoto kuwa fursa" alisema. Kwa upande wao, Watendaji Wakuu wa Kiwanda cha Uchakataji cha 'CHAKO' na Kikundi cha Ushirika cha 'Mungu Tuwafiki' kinachojihusisha na utengenezaji wa mbolea ya takataka, Bw. Suleiman Ali Mohamed na Mhe. Sulubu Kidombo Amour, wameiomba Serikali kuwawezesha ili waweze kupiga hatua kubwa zaidi. Katika ziara hiyo, Othman ametembelea Kiwanda cha CHAKO kinachojihusisha na uchakataji (recycling) wa chupa za vigae na plastiki na kuzitengeneza tena kuwa bidhaa za kitalii na majumbani, kilichopo Mndo Dole, Wilaya ya Magharibi 'B', Unguja. Pia aliyatembelea maeneo ya mashamba ya kilimo yanayoingia maji ya bahari huko Fungurefu, Mkokotoni; na Jaa la Kikundi cha 'Mungu Tuwafiki' kilichopo Matemwe, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Katika ziara hiyo, Othman aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Anna Athanas Paul, pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa, Wilaya, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (ZEMA).