SHEMDOE AONDOA ZUIO LA BAJAJI MBEYA ATOA AGIZO
ITV Tanzania
0:00 / 0:00
SHEMDOE AONDOA ZUIO LA BAJAJI MBEYA ATOA AGIZO
1 492 просмотра · 17 часов назад
ITV Tanzania
1,38 млн подписчиков
1 492 просмотра · 17 часов назад
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Profesa Riziki Shemdoe, ameondoa zuio la kutoingia kwa bajaji katika barabara kuu ya Tanzam jijini Mbeya, hatua hiyo inaambatana na maelekezo mahususi aliyompa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini.
Profesa Shemdoe amebainisha haya wakati wa ziara yake jijini humo na kumwelekeza Mkuu wa Mkoa kusitisha usajili wa bajaji mpya na kuagiza kuundwa kwa timu maalumu itakayochunguza mazingira ya vyombo vya moto, ikiwemo upangaji wa ruti. Waziri amebainisha kuwa idadi ya sasa ya bajaji 6,000 inatosha, wakati tathmini ya miundombinu ikiendelea.
Kadhalika amemtaka Mkuu wa Mkoa kufuatilia malalamiko dhidi ya uongozi uliopo madakarani wa Umoja wa Bajaji, ambao unakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na mali. Profesa Shemdoe ameagiza uongozi huo usimamishwe na badala yake uundwe uongozi wa muda wa mpito.
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ;
Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
Facebook : https://bit.ly/2KeQNl3
Twitter : https://bit.ly/2XG7aii
Instagram : https://bit.ly/34KItmg