MSAMIATI WA MAGONJWA/NDWELE/MARADHI
UKETO WA KISWAHILI TV (UWK TV)
0:00 / 0:00
MSAMIATI WA MAGONJWA/NDWELE/MARADHI
31 просмотр · 3 месяца назад
UKETO WA KISWAHILI TV (UWK TV)
112 подписчиков
31 просмотр · 3 месяца назад
MSAMIATI WA MARADHI/MAGONJWA/NDWELE
Homa Ugonjwa unaofanya joto la mwili kuwa juu kuliko kawaida (fever)
Mafua/bombo Ugonjwa wa kuambukizana unaomfanya mtu kuumwa na koo, kutokwa na kamasi na kuwa na homa (flu/cold)
Kikohozi Ugonjwa wa kifua unaomfanya mtu akohoe sana na kutoa balaghamu (cough)
Malaria Ugonjwa unaoambatana na homa kali unaoletwa na mbu.
Upele/kaga Vituruturu vilivyozagaa katika mwili na agh. Huwasha na kutunga usaha (scabies)
Kifafa Ugonjwa unaofanya mtu kuanguka na kupoteza fahamu kwa muda huku akipigapiga mikono na miguu na kutoa povu kinywani (epilepsy)
Kichocho Ugonjwa wa kukojoa damu unaosababishwa na vijidudu vikaavyo katika konokono wanaokaa katika maji baridi yaliyotuama. (bilharzia/schistosomiasis)
Mba/choa Ugonjwa wa ngozi ambao huwashana kuacha mabaka mwilini (dundruff).
Kifaduro Ugonjwa wa kukohoa sana na kutoa sauti kama ya filimbi agh. Huwashika watoto wadogo na huambukiza sana. (whooping cough)
Ukambi/Surua/shurua/firangi Ugonjwa wa kuambukiza agh unaowapata watoto, huifanya ngozi kuwa na vipele na unaoanza kwa kushikwa na homa kali ya kukohoa (measles)
Kipindupindu/waba Ugonjwa wa kuambukiza wa kuhara na kutapika sana (cholera).
Kifua Kikuu Ugonjwa wa kifua (Tb)
Majipu Uvimbe mkubwa unaotunga usaha (boil/abscess)
Tauni/kipukusa Ugonjwa wa homa kali unaoambukizwa na viroboto wa panya. (bubonic plague)
Koyo Kuvimba kwa miguu kunakompata mwanamke mjamzito (pre-eclampsia)
Ndui Ugonjwa wa kuambukiza unaofanana na surua, hutokeza pele nyingi zenye maji maji na usaha.(smallpox)
Malale Ugonjwa usingizi unaoambukizwa na mbung’o (sleeping sickness/trypanasomiasis).
Homa ya matumbo Taifoidi (typhoid)
Saratani/kansa Cancer
Matumbwitumbwi/machibwichibwi/perema/machapwi Ni ugonjwa wa kuvimba mashavu hadi chini ya taya hususana kwa watoto (mumps)
Rovu Ugonjwa wa kuvimba tezi kwenye shingo (goitre)
Tetekuwanga/tetemaji/galagala Ugonjwa wa pele na homa kali wa kuambukizwa agh kwa watoto. (chicken pox)
Hijabu/kiseyeye Ugonjwa wa kuvimba mafizi (gingivitis).
Pepopunda Ugonjwa unaosababishwa na bakteria unaopatikana katika kutu,vumbi au choo cha mnyama na kuingia kwenye jeraha. (Tetanus)
Kaswende/sekeneko/pangusa/farangi Ugonjwa unaoshika uke na uume na huambukizwa kwa njia ya ngono (syphilis).
Kisonono/kisalisali Ugonjwa wa zinaa wa kutokwa na damu au usaha kwenye tupu la mbele (gonorrhoea).
Unyafuzi/chirwa Ugonjwa wa watoto wa kutokuwa na afya njema kukosana na kukosa lishe (kwashiorkor)
Utapiamlo Ugonjwa unaowapata zaidi watoto kutokana na ukosefu wa viinilishe vya kutosha katika chakula (malnutrition)
Nyongea Ugonjwa wa watoto unaofanya mifupa ya miguu kuwa nyororo (rickets)
Kichomi/nimonia/mkamba Ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na bakteria wanaodhoofisha mfumo wa upumuaji. (pneumonia)
Safura/kung’uta Ugonjwa unaosababishwa na aina fulani ya michango unaomfanya mtu kukosa damu mwilini. (hookworm disease)
Matende Ugonjwa wa kuvimba unaosababishwa na aina mojawapo wa mbu (Elemphantiasis)
Pumu Ugonjwa wa mapafu unaomfanya mgonjwa awe na shida ya kupumua (asthma).
Banguzi (ulcers)
Kiharusi/faliji Ugonjwa wa kupooza viungo vya mwili wa binadamu na kuua hisi na nguvu za viungo hivyo (stroke).
Ukoma/jedhamu Ugonjwa wa kuambukiza wa mabatombato ambao unaharibu mishipa ya fahamu na kukata viungo vya mwili (leprosy).
Kekevu/chechevu Kwikwikwi inayosababishwa na kiungulia. (hiccup)
Mzio Allergy
Matege Bow-legs\
Ngiri Ugonjwa unaotokana na kukaza kwa mishipa iliyo sehemu za chini ya kitovu (hernia)
Kiyeye Ganzi la meno (sensitivity of the teeth)
Kisukari (Diabetes)