Niite Nirudi Kwetu | LADHA ZA GHASSANI
Gumzo la Ghassani
0:00 / 0:00
Niite Nirudi Kwetu | LADHA ZA GHASSANI
2 488 просмотров · 13 дн. назад
Gumzo la Ghassani
45,2 тыс. подписчиков
2 488 просмотров · 13 дн. назад
Niite Mama Niite, mwanao nirudi kwetu, nishachoka na safari
Niite kwetu nifike, kuliko na wetu watu, Niite wako swaghiri
Jamaa uwaalike, wajazane ndani mwetu, wanipokee kwa ari
Niite nirudi kwetu
Mama niite mwanao
Ishanichosha safari
Mama usiku inuka, umwambie Mola wetu, unamtaka mwanao
Mwanao nilokopoka, mwana nilohama Kwetu, hashika njia ambayo
Mbali ilonipeleka, kuso langu kuso letu, si kwa ndewe si sikio
Niite nirudi kwetu
Mama niite mwanao
Nishachoka kusafiri
Anitwaye anilete, kwa mawimbi ya bahari, na kwa pepo za musimu
Chomboni anifumbate, niiandame safari, nirudi kwenye isimu
Niite na niitike, na wala nisighairi, na wala nisilaumu
Niite nirudi kwetu
Mama niite mwanao
Nishachoka na safari
Nijile miye nijile, hima hima nije Kwetu
Nije kwa wangu wavyele, kwa nchi iliyo yetu
Nije kwenye mambo tele, yanofanya niwe mtu
Nije kwetu miye nije, Apendapo Mola wetu, nije pasina sumile!
Niite nirudi kwetu
Mama niite mwanao
Nishachoka na safari
Nije niyaone yote, ya kupwa na ya kujaa
Ya Chake Chake na Wete, ya Pandani na Wambaa
Nami nionwe na wote, marafiki na jamaa
Nije kwetu miye nije, Neema au fadhaa, Ya kwetu ni yetu sote
Niite nirudi kwetu
Mama niite mwanao
Nishachoka na safari
Nije na nije kikweli, mwendakwao si mtovu
Nije wala nisijali, wapi palipo pabovu
Nije na yangu akili, na ilimu na welevu
Nije kwetu miye nije, Niwajiao ni wangu, Na miye pia ni wao
Niite nirudi kwetu
Mama niite mwanao
Nishachoka na safari
Nije kwenu mama na baba, kwa babu na bibi zangu
Nije kunako mahaba, fakhari na gambo langu
Ningakumbwa na adhaba, kwavyo huko kuja kwangu
Nije kwetu miye nije, Ndio uamuzi wangu, Lolote nitalibeba
Niite nirudi kwetu
Mama niite mwanao
Nishachoka na safari
Basi zifise salamu, uwaonapo jamaa
Wambe punde utatimu, muda wa kushika njia
Na hilo nishaazimu, na nyuma sitarejea
Naja kwetu miye naja, Naja hali ‘meridhia, Kuwa na yangu kaumu
Niite nirudi kwetu
Mama niite mwanao
Nishachoka na safari