ASKOFU DKT. MSAFIRI MBILU HURUMA YA KRISTO IONEKANE KWA VITENDO.
KKKT DKMS Online TV
0:00 / 0:00
ASKOFU DKT. MSAFIRI MBILU HURUMA YA KRISTO IONEKANE KWA VITENDO.
138 просмотров · 6 дней назад
KKKT DKMS Online TV
9,47 тыс. подписчиков
138 просмотров · 6 дней назад
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesisitiza kuwa huruma ya Yesu Kristo ni endelevu katika maisha ya waumini, akiwataka Wakristo kuonyesha huruma hiyo kwa vitendo, hasa kwa kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali katika jamii.
Akihubiri katika Ibada ya Jumapili iliyofanyika Jimbo la Pwani Usharika wa Pongwe, Askofu Dkt. Mbilu ametumia tukio la Yesu kuwalisha watu kwa mikate saba na samaki wachache kufundisha kuwa Mungu anawahurumia wahitaji na anaweza kutumia kile kidogo kilichopo kufanya jambo kubwa.
“Huruma ya Kristo haipaswi kubaki katika maneno pekee, bali ionekane kwa matendo katika maisha yetu ya kila siku,” amesisitiza Askofu Dkt. Mbilu.
Tufuatilie kupitia:
📘 Facebook Account: North Eastern Diocese
📘 Facebook Page: ELCT – North Eastern Diocese
▶️ YouTube: KKKT DKMS Online TV
🌐 Website: www.elctned.org