WAKALA WA VIPIMO WATOA ELIMU KIWANDA CHA KUFUNGASHA PARACHICHI NJOMBE
Mchuchuma tv
0:00 / 0:00
WAKALA WA VIPIMO WATOA ELIMU KIWANDA CHA KUFUNGASHA PARACHICHI NJOMBE
202 просмотра · 1 месяц назад
Mchuchuma tv
8,3 тыс. подписчиков
202 просмотра · 1 месяц назад
WAKALA WA VIPIMO WATOA ELIMU NJOMBE KUHUSU MATUMIZI SAHIHI YA VIPIMO
Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA), Albogust Kajungu, amesema lengo la ziara yao mkoani Njombe ni kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya vipimo kwa wauzaji, wanunuzi na wazalishaji ili kuhakikisha kila mmoja anazingatia vipimo vilivyowekwa kisheria na kuondoa unyonyaji katika biashara.
Wakala huo umeendelea kusisitiza umuhimu wa kutumia mizani na vifaa vya kupimia vilivyohakikiwa na kuthibitishwa kwa mujibu wa sheria, hatua inayolenga kulinda haki za walaji, kuimarisha uwazi katika biashara na kujenga imani kati ya wauzaji na wanunuzi.
Zoezi la utoaji wa elimu lilianza tarehe 30 Julai na linatarajiwa kukamilika tarehe 2 Agosti, likiwahusisha viongozi wa serikali za mitaa, wakiwemo madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa, kwa lengo la kuweka msingi imara wa uelewa wa sheria za vipimo kwa wananchi.