Перейти к содержимому

MWENYEKITI WA WAJUMUIYA YA WAFANYABIASHARA KARIAKOO AFUNGUKA MAZITO MBELE YA MGENI RASMI ASEMA....

JAMBO TV

0:00 / 0:00

MWENYEKITI WA WAJUMUIYA YA WAFANYABIASHARA KARIAKOO AFUNGUKA MAZITO MBELE YA MGENI RASMI ASEMA....

1 397 просмотров · 9 ч назад
JAMBO TV
1,12 млн подписчиков
1 397 просмотров · 9 ч назад
#JAMBOTV WAFANYABIASHARA KARIAKOO WALALAMIKIA KODI YA TAKA, MEZA ZA MACHINGA Wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam wameiomba Serikali kutatua changamoto ya kutozwa kodi ya taka kwa duka na stoo inayotumika kuhifadhi bidhaa za biashara hiyo hiyo, pamoja na uwepo wa meza za wafanyabiashara katika maeneo ya mbele ya maduka na njia za kupita. Akizungumza katika kikao kati ya wafanyabiashara na Serikali wilayani humo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Severine Mushi, amesema wafanyabiashara hawapingi uwepo wa machinga, bali wanataka biashara zifanyike kwa utaratibu bila kuathiri shughuli zao. Ameomba pia njia za kupita ziachwe wazi ili kurahisisha upatikanaji wa wateja na usafirishaji wa mizigo. Akijibu hoja hizo, Katibu Tawala wa Wilaya, Charangwa Selemani Makwiro, amesema Serikali itakutana na mkandarasi wa huduma ya taka ili kutatua suala la kodi hiyo, huku akisema wafanyabiashara watapata majibu ndani ya wiki moja hadi mbili. Amesema pia doria za usiku zinaendelea kwa ajili ya kuimarisha usalama na utaratibu wa biashara Kariakoo. ........... Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii ►YOUTUBE:    / @jambotv908   ►INSTAGRAM:   / jambotv   ►TWITTER:   / jambotv_   ►FACEBOOK:   / jambotv   ►WEBSITE: https://jambo.tz/