WADAU WA ELIMU WAJITOKEZA KWENYE KONGAMANO LA NNE LA KITAIFA LA HUDUMA ZA MAKTABA.
Esbn Tv
0:00 / 0:00
WADAU WA ELIMU WAJITOKEZA KWENYE KONGAMANO LA NNE LA KITAIFA LA HUDUMA ZA MAKTABA.
15 просмотров · 3 дн. назад
Esbn Tv
52 подписчика
15 просмотров · 3 дн. назад
HITIMISHO LA KONGAMANO LA MABORESHO YA HUDUMA ZA MAKTABA
Kongamano la Maboresho ya Huduma za Maktaba limehitimishwa leo, tarehe 22 Oktoba 2026, kwa mafanikio, baada ya kuanza tarehe 20 Oktoba 2026.
Kongamano hilo limekuwa jukwaa muhimu la kujadili mikakati ya kuboresha upatikanaji wa huduma za maktaba, kuimarisha matumizi ya teknolojia katika upatikanaji wa taarifa, pamoja na kukuza utamaduni wa kusoma katika jamii.
Aidha, kongamano hilo limetoa fursa kwa washiriki kubadilishana uzoefu, mawazo na mapendekezo yatakayochangia kuboresha huduma za maktaba ili ziendane na mahitaji ya wananchi katika zama za sasa.
Kuhitimishwa kwa kongamano hili ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma za maktaba na kukuza jamii yenye utamaduni wa kusoma, kupata maarifa na kutumia taarifa kwa maendeleo endelevu.
Wadau tofauti tofauti wa Elimu na Taasisi mbalimbali pamoja na Wanafunzi kutoka Shule mbali mbali walijitokeza kushiriki na kupata Elimu na Ujuzi wa Mfumo mpya wa usomaji Vitabu Kidijitali.
Maktaba bora, maarifa zaidi, maendeleo kwa wote.
#maktaba #habari #kongamano #uongozi
#tlsbupdates2026 #maktabakidijitalinaujuzikwadira2050 #esbntv #educate #information