Перейти к содержимому

BIASHARA ZISIZO RASMI DARAJANI ZIONDOLEWA, RC MJINI ATOA MAELEKEZO

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

BIASHARA ZISIZO RASMI DARAJANI ZIONDOLEWA, RC MJINI ATOA MAELEKEZO

10 965 просмотров · 2 дня назад
ASAM Online TV
22,2 тыс. подписчиков
10 965 просмотров · 2 дня назад
Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Dkt. Said Haji Mrisho, ameongoza zoezi la kuondoa biashara zinazofanyika katika maeneo yasiyo rasmi na kinyume na utaratibu katika eneo la Darajani. Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Dkt. Said amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wenye maduka katika Soko la Darajani, ambao wamekuwa wakilalamikia biashara zinazofanyika nje ya maeneo rasmi yaliyotengwa. Amesema biashara zinazofanyika nje ya maeneo yaliyotengwa zinaathiri mpangilio wa eneo la soko na hivyo hatua hiyo inalenga kurejesha utaratibu katika eneo hilo. Dkt. Said amesema zoezi hilo ni endelevu, huku akiwataka viongozi wengine kuendelea kusimamia utekelezaji wa utaratibu huo. Amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha Soko la Darajani linabaki katika hali nzuri, lenye mpangilio na mazingira yanayokubalika kwa wafanyabiashara pamoja na wananchi wanaofika katika eneo hilo. #AsamOnlineTV #ZanzibarNews #HabariZanzibar #Darajani #Biashara #SokoLaDarajani #NewsUpdate #Zanzibar