Перейти к содержимому

MAHAKAMA YATOA HUKUMU, OFISI YA MUFTI ITAENDELEA KUWA CHINI YA SERIKALI

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

MAHAKAMA YATOA HUKUMU, OFISI YA MUFTI ITAENDELEA KUWA CHINI YA SERIKALI

8 043 просмотра · 11 мес. назад
ASAM Online TV
22,6 тыс. подписчиков
8 043 просмотра · 11 мес. назад
Mahakama Kuu ya Tunguu, Zanzibar imetoa uamuzi wa kukataa rufaa iliyowasilishwa na masheikh wa Zanzibar waliopinga uwepo wa Ofisi ya Mufti ndani ya Serikali, wakidai kuwa sheria inayounda ofisi hiyo inakinzana na Katiba ya Zanzibar. Katika hukumu iliyosomwa mbele ya majaji watatu—Mheshimiwa Said Hassan, Mheshimiwa Haji Suleiman na Mheshimiwa Salum Hassan Bakar—mahakama imeeleza kuwa sheria hiyo haiendi kinyume na Katiba na haina kipengele chochote cha ubaguzi, hivyo madai ya walalamikaji hayana mashiko ya kisheria. Akizungumza na Asam TV mara baada ya hukumu hiyo, wakili wa upande wa walalamikaji, Hassan Kijogoo, amesema wanaheshimu uamuzi wa mahakama, lakini wataendelea na jitihada za kutafuta haki kwa kuipeleka kesi hiyo Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).