WAFANYABIASHARA WALIOVAMIA HIFADHI ZA BARABARA WAONYWA
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
WAFANYABIASHARA WALIOVAMIA HIFADHI ZA BARABARA WAONYWA
4 383 просмотра · 1 день назад
ASAM Online TV
22,6 тыс. подписчиков
4 383 просмотра · 1 день назад
Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Dkt. Said Haji Mrisho, amefanya ziara ya kukagua hali ya usafi katika barabara kuu za wilaya hiyo, ikiwemo Maisara, Mazizini, Jang’ombe na Mwanakwerekwe Roundabout.
Ziara hiyo imelenga kuimarisha usafi wa mazingira, kupanga upya shughuli za kibiashara na kuwaondoa wafanyabiashara waliovamia maeneo ya pembezoni mwa barabara ili kurejesha muonekano mzuri wa maeneo hayo na kuimarisha nidhamu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa ya Mjini, Hasna Attai Massoud, amewataka wananchi na wafanyabiashara kushirikiana katika kutunza mazingira ili kuhakikisha manispaa hiyo inabaki safi wakati wote.
Amesema uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi kuhusu umuhimu wa usafi bado ni changamoto, akisisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaokaidi maagizo yaliyowekwa.
#AsamOnlineTV #ZanzibarNews #UsafiWaMazingira #Zanzibar