Ajali dodoma
Galaxy Media
0:00 / 0:00
Ajali dodoma
27 просмотров · 10 дн. назад
Galaxy Media
297 подписчиков
27 просмотров · 10 дн. назад
Dereva wa basi la Kampuni ya Satco, Juma Mohamed (40), amefariki dunia baada ya basi alilokuwa akiendesha kugongana na lori, kuacha njia na kugonga mti eneo la Msembeta, Dodoma. Ajali hiyo imetokea leo, Septemba 8, 2026, majira ya saa 12:20 asubuhi katika barabara ya Dodoma-Singida.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP Gallus Hyera, amesema basi hilo lenye namba T 115 EQD lilikuwa likitokea Bukoba kuelekea Dodoma lilipogonga ubavuni mwa lori aina ya DAF, lenye namba T 834 EEE na tela T 161 CUX, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mpanda.
Amesema watu watatu walijeruhiwa na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambapo uchunguzi wa awali umebaini ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa dereva wa basi kushindwa kulimudu gari, huku madereva wakitakiwa kuzingatia usalama barabarani.