HIVI NDIVYO WATEJA WA BENKI WANAVYOWIBIWA – KAMANDA MAIGWA
Mwananchi Digital
0:00 / 0:00
HIVI NDIVYO WATEJA WA BENKI WANAVYOWIBIWA – KAMANDA MAIGWA
2 799 просмотров · 10 ч назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
2 799 просмотров · 10 ч назад
Moshi.Wateja wanaotoa kiasi kikubwa cha fedha benki mkoani Kilimanjaro wameonywa kuwa makini baada ya Polisi kubaini mbinu mpya inayodaiwa kutumiwa na wahalifu kuwafuatilia na kuwaibia baada ya kutoka benki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Simon Maigwa amesema hayo leo mjini Moshi wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja ya Benki ya Azania, akisema wahalifu hao huwafuatilia wateja hadi wanapokwenda kupata huduma nyingine.
Amesema wahalifu hao hawawavamii wateja ndani ya benki, bali huwafuatilia hadi maeneo kama migahawani au sehemu nyingine za mapumziko, kisha kuwaibia fedha walizochukua. “Mtu hakuvamii benki lakini anaangalia umechukua fedha na anakufuatilia,” amesema.
Maigwa amesema Polisi imeanza kusambaza namba maalum za simu katika benki ili mteja anayechukua au kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha aweze kuomba msaada wa haraka, ikiwamo ulinzi wa Polisi.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha ushirikiano kati ya Polisi, benki na wananchi katika kuzuia uhalifu huo, huku akiwataka wateja kutoa taarifa wanapomtilia mtu shaka au wanapohitaji ulinzi baada ya kutoa fedha nyingi.