WASWAHILI WANASEMA KIPAJI HAKIKUI KWA BAHATI MBAYA BALI HUKUA KWA BIDII MAALIFA NA NIDHAMU!
Mvula Sports
0:00 / 0:00
WASWAHILI WANASEMA KIPAJI HAKIKUI KWA BAHATI MBAYA BALI HUKUA KWA BIDII MAALIFA NA NIDHAMU!
30 просмотров · 1 месяц назад
Mvula Sports
6,33 тыс. подписчиков
30 просмотров · 1 месяц назад
Shakia Said Kibode, ni miongoni mwa vijana wenye vipaji na wanaotarajiwa kufanya vizuri kutoka Mvula Sports Academy, ambaye pia anapata mafunzo maalum ya kukuza kipaji kupitia Kituo cha TFF cha Maendeleo ya Vipaji Kigamboni.
Kinachomtofautisha Shakia ni kwamba haridhiki na mazoezi ya kawaida pekee. Baada ya kutoka shuleni, kila Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi na Ijumaa, hutenga muda wa ziada kufanya mazoezi binafsi ili kujijenga zaidi na kuimarisha uwezo wake.
Kisha kila Jumamosi na Jumapili, hujiunga na wenzake katika Kituo cha TFF Kigamboni kwa ajili ya kuendelea kuendeleza na kunoa kipaji chake.
Hii ndiyo tafsiri halisi ya nidhamu, kujituma na kuwa na ndoto kubwa. Mafanikio huanza pale unapokuwa tayari kufanya zaidi ya kile kinachotarajiwa kutoka kwako.
🎥 Tazama video hii, kisha msikilize Shakia mwenyewe akieleza dhamira yake ya kuwa miongoni mwa wanasoka wakubwa wa Tanzania na kuipeperusha bendera ya Taifa katika medani ya kimataifa.
Mvula Sports Academy – Kulea, Kukuza na Kuendeleza Vipaji vya Michezo kwa Mafanikio ya Baadaye. ⚽🇹🇿
#MvulaSportsAcademy #TFF #Kigamboni #FutureStar #FootballDevelopment #Discipline #HardWork #DreamBig #TanzaniaFootball