MWANACHAMA WA KIKUNDI KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KWA SHILINGI ELFU 60,000
Uyui FM Radio
0:00 / 0:00
MWANACHAMA WA KIKUNDI KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KWA SHILINGI ELFU 60,000
76 просмотров · 4 дн. назад
Uyui FM Radio
21,7 тыс. подписчиков
76 просмотров · 4 дн. назад
Wananchi, hususani wajasiriamali wadogo wakiwemo wamachinga, waendesha bodaboda, mama na baba lishe wametakiwa kuona umuhimu wa kutumia fursa ya kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote kupitia vikundi vyao, ambapo kila mwanachama atalipia shilingi elfu 60 kwa mwaka.
Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Tabora, Raphael Francis Malaba, amesema mpango huo unalenga kuhakikisha kila Mtanzania anapata uhakika wa matibabu bila kuathiri kipato chake.
Amesema kwa mkoa wa Tabora, awamu ya pili inalenga kusajili kaya 23,773 zenye jumla ya wanufaika 57,129, huku Manispaa ya Tabora ikilenga kaya 1,187.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Manispaa ya Tabora, Asha Churu, amesema afya ni msingi wa maendeleo ya mtu binafsi, familia na jamii kwa ujumla, akieleza kuwa gharama za matibabu zinaweza kuathiri uchumi wa familia husika.
Baadhi ya wawakilishi wa vikundi vya kijamii wameipongeza Serikali kwa kuanzisha mpango huo unaowapa nafasi wajasiriamali wadogo kupata huduma za afya kwa gharama nafuu.
Wamesema utaratibu wa kuchangia shilingi elfu 60 kwa mwanachama kupitia kikundi utasaidia kupunguza mzigo wa gharama za matibabu.
📻 Sikiliza Uyui FM Radio popote ulipo duniani, bofya kiungo (link) kwenye bio yetu.
#2026Fanikisha #tunasambazaunyamwezi #Fanikisha #radioyetusautiyetu