Перейти к содержимому

Je Lini Tarehe YA Matarajio ya Ujauzito kwa Ultrasound ni sahihi zaidi? (Je Ultrasound huwa sahihi?)

Dr. Mwanyika

0:00 / 0:00

Je Lini Tarehe YA Matarajio ya Ujauzito kwa Ultrasound ni sahihi zaidi? (Je Ultrasound huwa sahihi?)

25 086 просмотров · 4 г. назад
Dr. Mwanyika
230 тыс. подписчиков
25 086 просмотров · 4 г. назад
Matazamio yakujifungua, Matarajio ya Ultrasound yakujifungua, Matazamio yakujifungua, Matarajio,Matarajio ya kujifungua kwa kutumia ultrasound na Matarajio ya kujifungua kwa Mjamzito. Bonyeza link hii hapa chini ili kusubscribe channel hii https://bit.ly/3zQ3IU0 ULTRASOUND NA TAREHE YA MATARAJIO. Ultrasound hutumika kuangalia Mambo mengi sana kwa Mjamzito. Mojawapo ya Mambo ya Msingi ambayo Ultrasound hutumika kuangalia ni Tarehe ya Matarajio au Matazamio. Ultrasound inapofanyika Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito, Mimba ya kuanzia na chini ya wiki 13 na siku 6 huwa na majibu sahihi zaidi ya Tarehe ya Matarajio kuliko kipindi chochote cha Ujauzito. Ultrasound ikifanyika kuanzia Miezi 4 ya Ujauzito huwa na majibu tofauti na Uhalisia hii ni kwa sababu umri wa Mimba unavyoongezeka majibu ya Ultrasound huwa na tofauti kubwa ukilinganisha na Tarehe ya Matarajio kutokana na siku ya kwanza ya Hedhi ya mwisho. MAMBO YANAYOWEZA KUATHIRI TAREHE YA MATARAJIO KUTOKA NA ULTRASOUND. Pamoja na kwamba Ultrasound huwa na majibu sahihi katika kipindi cha Mwanzoni mwa Ujauzito, Majibu yake huweza kuwa na tofauti kubwa kutokana na sababu zifuatazo: 1. Umri wa Mimba/Ujauzito. Kadiri umri wa Mimba unavyoongezeka ndivyo utofauti wa Tarehe ya Matarajio ya Ultrasound na Tarehe ya Matarajio kutokana na hedhi yako ya mwisho huongezeka. 2. Ujuzi wa Mtu anayefanya Ultrasound. Tarehe ya Matarajio ya Ultrasound huwa na Uhalisia au kweli zaidi endapo mtu anayefanya Ultrasound ana Ujuzi wa kutosha kuhusu Ultrasound na Upimaji endapo hana Ujuzi wa kutosha majibu huwa ya tofauti kubwa zaidi. 4. Ubora wa Mashine. Mashine Bora hutoa majibu ya tarehe ya matarajio sahihi zaidi ukilinganisha na Tarehe ya Matarajio kutokana na hedhi ya mwisho tofauti na hapo huwa na majibu ambayo si sahihi. 4. Mkao wa Mtoto. Endapo Mtoto amekaa vibaya huwa ni ngumu kupata Tarehe ya Matarajio kutokana na Ultrasound ambayo ni sahihi zaidi. ULINGANISHAJI WA TAREHE YA MATARAJIO KUTOKA NA ULTRASOUND DHIDI YA TAREHE YA MATARAJIO KUTOKANA NA HEDHI YA MWISHO. Hapa nitakuwa naonesha utofauti wa Tarehe ya Matarajio ya Ultrasound na Tarehe ya Matarajio kutokana na hedhi ya mwisho kulingana na umri wa Ujauzito. 1. MIMBA YA CHINI YA WIKI 13 NA SIKU 6(MIEZI 3 WIKI 1 NA SIKU 6). Endapo ukilinganisha tarehe ya matarajio kutokana na ultrasound na ile ya hedhi yako ya mwisho, Kwa kawaida ultrasound huzidisha au kupunguza siku 7. (±7) Kuna makundi makuu mawili kutokana na Umri wa Mimba/Ujauzito. a. Mimba ya Umri chini ya Wiki 8 na siku 6. Tarehe ya Matarajio ya Ultrasound ukilinganisha na Tarehe ya Matarajio kutokana na hedhi ya mwisho. Kwa kawaida Ultrasound huweza kuzidisha au kupunguza siku 5 (±5) b. Mimba ya wiki 9(Miezi 2 na wiki1) Hadi wiki 13 na siku 6(Miezi 3, Wiki 1 na Siku 6) Endapo ukilinganisha tarehe ya matarajio kutokana na ultrasound na ile ya hedhi yako ya mwisho, Kwa kawaida ultrasound huzidisha au kupunguza siku 7. (±7) 3. Mimba ya Wiki 14 (Miezi 3 na wiki 2) hadi Wiki 15 na siku 6 (Miezi 3, Wiki 2 na Siku 6). Endapo ukilinganisha tarehe ya matarajio kutokana na ultrasound na ile ya hedhi yako ya mwisho, Kwa kawaida ultrasound huzidisha au kupunguza siku 7(±7). 4. Mimba ya Wiki 16 (Miezi 4) hadi hadi Wiki 21 na siku 6 (Miezi 5 wiki 1 na siku 6) Endapo ukilinganisha tarehe ya matarajio kutokana na ultrasound na ile ya hedhi yako ya mwisho, Kwa kawaida ultrasound huzidisha au kupunguza siku 10 (±10). 5. Mimba ya wiki 22 (Miezi 5 na wiki 2) hadi wiki 27 na siku 6 (Miezi 6 Wiki 3 na siku 6) Endapo ukilinganisha tarehe ya matarajio kutokana na ultrasound na ile ya hedhi yako ya mwisho, Kwa kawaida ultrasound huzidisha au kupunguza siku 14 au Wiki 2. (±14) 6. Mimba ya wiki 28 (Miezi 7) kwenda juu. Endapo ukilinganisha tarehe ya matarajio kutokana na ultrasound na ile ya hedhi yako ya mwisho, Kwa kawaida ultrasound huzidisha au kupunguza siku 21 au wiki 3. (±21). Hivyo Tarehe ya Matarajio ya Ultrasound hutofautiana zaidi na Tarehe ya Matarajio kutokana na hedhi ya mwisho endapo umri wa Mimba ni mkubwa zaidi. Endapo ulifanya Ultrasound zaidi ya Mara moja au Mbili ni vema kutumia Tarehe ya Matarajio ya Ultrasound ambayo ilifanyika kwa Mara ya kwanza Mimba ilipokuwa katika Umri mdogo zaidi. Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito.    / drmwanyika   Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito.   / japideafya   Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/de... #EDDyaUltrasound #DrMwanyika #MamaAfya