Перейти к содержимому

RC NYONGO: TUOMBE MUNGU ATUEPUSHE NA MAFURIKO...

Habari Na Zaidi

0:00 / 0:00

RC NYONGO: TUOMBE MUNGU ATUEPUSHE NA MAFURIKO...

133 просмотра · 4 дн. назад
Habari Na Zaidi
68 подписчиков
133 просмотра · 4 дн. назад
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Stanslaus Nyongo, amewasihi wakazi wa Wilaya ya Kisarawe na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kumuomba Mungu awapitishe salama na kuwaepusha na madhara yanayoweza kusababishwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha. Mhe. Nyongo ameyasema hayo Oktoba 6, 2026, wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Homboza, Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, ambapo alisikiliza na kujibu kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa eneo hilo. Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema kwa kuhifadhi chakula cha kutosha, kuzingatia taarifa za mamlaka kuhusu hali ya hewa na, pale inapobidi, kuhama maeneo hatarishi hususan maeneo ya mabondeni yanayoweza kuathiriwa na mafuriko. Aidha, amewasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanalindwa na kuepuka maeneo hatarishi wakati wa mvua kubwa, huku akiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.