Перейти к содержимому

"HATUTAKAA KWENYE VITI VYA KUZUNGUKA" - DKT NASRA

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

"HATUTAKAA KWENYE VITI VYA KUZUNGUKA" - DKT NASRA

3 001 просмотр · 21 ч назад
ASAM Online TV
22,3 тыс. подписчиков
3 001 просмотр · 21 ч назад
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Dkt. Nasra Nassor, amesema yupo tayari kushirikiana na watendaji wa Wizara hiyo katika kuimarisha na kukuza sekta ya utalii nchini Zanzibar. Dkt. Nasra ameyasema hayo leo katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni, Zanzibar, wakati akikabidhiwa rasmi ofisi hiyo na aliyekuwa Kaimu Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga. Amesema ushirikiano kati ya viongozi na watendaji wa Wizara ni muhimu katika kuhakikisha majukumu yanatekelezwa kwa ufanisi na malengo ya kuendeleza sekta ya utalii yanafikiwa. Kwa upande wake, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amewataka watendaji wa Wizara hiyo kuweka pembeni tofauti zao na kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao, ili kuhakikisha Wizara inafikia malengo yaliyowekwa na kuchangia maendeleo ya sekta ya utalii Zanzibar. Amesema mshikamano na ushirikiano wa watendaji ni miongoni mwa mambo muhimu katika kuhakikisha sekta ya utalii inaendelea kutoa mchango katika maendeleo ya Zanzibar. #AsamOnlineTV #ZanzibarNews #HabariZanzibar #UtaliiZanzibar #NasraNassor #Utalii #MamboYaKale #ZanzibarTourism #Kikwajuni #NewsUpdate #Trending