Перейти к содержимому

NDC–TZ YARIDHISHWA NA MABORESHO BANDARI YA TANGA #MWAMBELAINFO

MWAMBELA TV

0:00 / 0:00

NDC–TZ YARIDHISHWA NA MABORESHO BANDARI YA TANGA #MWAMBELAINFO

208 просмотров · 9 мес. назад
MWAMBELA TV
6,2 тыс. подписчиков
208 просмотров · 9 мес. назад
NDC–TZ YARIDHISHWA NA MABORESHO YA BANDARI TANGA ‎ ‎Imeelezwa kuwa maboresho makubwa yaliyofanywa katika Bandari ya Tanga yameleta tija katika sekta ya usafirishaji na kuchochea ukuaji wa uchumi katika mikoa ya Kaskazini na Kaskazini Mashariki mwa Tanzania pamoja na nchi jirani. ‎ ‎Akizungumza wakati wa ziara ya mafunzo kwa vitendo ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania (NDC–TZ), Brigedia ‎Jenerali Baganchwera Rutambuka amesema upanuzi wa gati na uboreshaji wa miundombinu umeongeza ufanisi wa utoaji huduma, hali iliyopelekea kuongezeka kwa idadi ya meli, shehena za mizigo, mapato ya bandari pamoja na kupungua kwa muda wa kushusha mizigo. ‎ ‎Brigedia Jenerali Rutambuka ameongeza kuwa Bandari ya Tanga ina nafasi ya kipekee ya kuwa kitovu muhimu cha usafirishaji kwa ukanda wa Kaskazini endapo maboresho yataendelea kufanyika, akibainisha kuwa ni bandari muhimu inayohudumia maeneo mengi ya kanda hiyo. Comment Like Share Subscribe #MWAMBELAINFO