Rc Kunenge, amewapongeza wafanyakazi kwa bidii na weledi wao uliosaidia mkoa huo kuongoza katika mae
Habari Na Zaidi
0:00 / 0:00
Rc Kunenge, amewapongeza wafanyakazi kwa bidii na weledi wao uliosaidia mkoa huo kuongoza katika mae
89 просмотров · 5 мес. назад
Habari Na Zaidi
68 подписчиков
89 просмотров · 5 мес. назад
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amewapongeza wafanyakazi kwa bidii na weledi wao uliosaidia mkoa huo kuongoza katika maendeleo. Amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika Bagamoyo.
Ameeleza kuwa anatambua mchango wa watumishi, akibainisha kuwa juhudi zao zimewezesha mkoa kuwa na viwanda 1,722 na kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato.
Pia amesema utendaji huo umechangia viwanda 57 kukua na kuanza kulipa kodi katika makao makuu, ishara ya maendeleo ya kiuchumi.
Aidha, ameahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kazi na kushughulikia changamoto za watumishi ili kuongeza ufanisi wao.