WATU WAWILI WAUAWA TINDIGA, WANANCHI WAOMBA MSAADA
CLOUDS HABARI
0:00 / 0:00
WATU WAWILI WAUAWA TINDIGA, WANANCHI WAOMBA MSAADA
157 просмотров · 1 день назад
CLOUDS HABARI
1,92 тыс. подписчиков
157 просмотров · 1 день назад
WATU WAWILI WAUAWA TINDIGA, WANANCHI WAOMBA MSAADA
Watu wawili, Festo Selias Chaula na Kelvin Mhagama, wakazi wa Kata ya Tindiga wilayani Kilosa mkoani Morogoro, wamefariki dunia kwa nyakati tofauti kufuatia mzozo mkali wa ardhi uliogeuka kuwa ghasia kubwa Septemba 23, 2026.
Wakielezea kiini cha mkasa huo, wakazi wa kijiji cha Tindiga na Malui wamesema Chaula alivamiwa na kukatwa mapanga kichwani akiwa shambani kwake, baada ya kujaribu kuwazuia wafugaji kupitisha mifugo kwenye shamba lake alilokuwa akiliandaa kwa ajili ya kilimo cha nyanya, ambapo alifariki akipatiwa matibabu hospitali ya wilaya ya Kilosa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Andrew Kantimbo ameeleza kuwa watu wawili wamekamatwa ambao ni Seletwi Mdamanya na Paulo Sumai kwa mauaji ya mwanzo, huku likidai kuwa askari watatu walijeruhiwa na gari pamoja na pikipiki za doria viliharibiwa vibaya kwenye ghasia hizo.
@damalimagai
#Cloudsdigitalupdates
#Morogoro