MHE. HEMED ANZANIA INAHITAJI WAHANDISI WABOBEZI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO.
CTV NEWS TANZANIA
0:00 / 0:00
MHE. HEMED ANZANIA INAHITAJI WAHANDISI WABOBEZI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO.
34 просмотра · 3 недели назад
CTV NEWS TANZANIA
125 подписчиков
34 просмотра · 3 недели назад
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Tanzania inatambua kuwa Uhandisi ndio kiini cha Ajenda ya Maendeleo ya Kitaifa katika uwekezaji wa Miundombinu mbalimbali inayohitaji wahandisi wabobezi wenye utayari wakuijenga Tanzania yenye miundombinu imara itakayodumu kwa muda mrefu.
Ameyasema hayo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi katika hafla ya Ufunguzi wa Wiki ya 12 ya Uhandisi wa Afrika ya UNESCO unaofanyika sambamba na Mkutano wa Kumi (10) wa Uhandisi wa Afrika 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Amesema Mustakbali wa Afrika utajengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali, wahandisi, wasomi, washirika wa Maendelo na Jamii kwa ujumla kwa kubadilishana maarifa, uzoefu na ujuzi ambavyo ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa Taifa na kuboresha maisha ya watu.
Makamu wa Pili wa Rais amewataka wahandisi kuangalia namna ya kuimarisha elimu ya uhandisi na kuharakisha matumizi ya Teknolojia yatakayoongeza fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali pamoja na kuunda fursa kwa wahandisi wanawake na vijana watakaoimarisha zaidi utafiti, uvumbuzi na biashara kupitia taaluma ya Uhandisi.
Mhe. Hemed amebaisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuekeza katika miradi mikubwa ya Kimkakati ikiwemo ujenzi wa Bandari, Viwanja vya ndege, miundombinu ya maji na umeme, utalii na viwanda ambayo inaonesha wazi kuwa Taaluma ya Uhandisi ni kichocheo cha utekelezaji wa miradi hio.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema katika kuadhimisha Wiki ya Uhandisi Barani Afrika wahandisi wanapaswa kuweka msisitizo katika kuwanyanyua wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalumu kwa kuwajengea uwezo katika masomo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi pamoja na kuwatengenezea mazingira wezeshi wahandisi wanawake katika kushika nafasi za uongozi na kufikia ngazi za kutoa maamuzi.
Hata hivyo amewasisitiza wahandisi kufanyakazi kwa pamoja na kuwa tayari kuitumia taaluma ya uhandisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye matokeo chanya yanayoweza kuchangia maendeleo ya Taifa, Kikanda na Bara la Afrika kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Ujenzi Tanzania Mhe. Mhandisi GODFREY KASEKENYA amesema Tasnia ya Uhandisi inatambulika kama daraja la kufikia maendeleo katika nyanja ya uchumi na jamii hasa katika kuelekea uwekezaji Mkubwa wa miradi ya Kimkakati inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mhe. Kasekenya amefahamisha kuwa Tanzania katika kufikia maendeleo endelevu inahitaji kuekeza zaidi katika Tasnia ya Uhandisi itakayozalisha wahandisi wabobezi ambao wataisaidia serikali katika kubuni, kuvumbua na kujenga majengo yenye viwango vya hali ya juu.
Aidha, Kasekenya amewashauri wahandishi kuzidisha ushirikiano wa karibu na Serikali, wasomi, washirika wa maendeleo na wahandisi wa ndani na nje ya nchi ili kuiwezesha Tasnia ya uhandisi kuimarika zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Kwa upande wake Raisi wa Shirikisho la Wahandisi Afrika Mhandisi REFILWE BUTHELEZI amesema Teknoloji, ujuzi, ufundi na uvumbuzi vinaiweka pamoja Tasnia ya Uhandisi na wahandisi wenyewe katika kutimiza malengo ya Taaluma hio.
Mhandisi BUTHELEZI amewataka wahandisi kulitumia vyema juma la Uhandisi Afrika kwa kutafakari fursa za masoko kwa wahandisi, kuondosha kasoro zilizopo katika kada ya Uhandisi na kuwa tayari kufanya mabadiliko makubwa katika matumizi ya Teknolojia.
Mwakilishi kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO ) Dkt. YUSLAN NOR amesema kuna pengo kubwa katika Taaluma ya uhandisi ambalo litazibwa kwa kuongeza idadi ya wahandisi, ubunifu katika matumizi ya Teknolojia pamoja na kutengeneza Sera nzuri zitakazowavutia wawekezaji ambao watahitaji wahandisi katika uwekezaji wao.
Dkt. NOR ameipongeza Taasisi ya Wahandisi Tanzania kwa kuandaa Mkutano wa Wiki ya Uhandisi Afrika utakaowajengea uwezo, ujuzi na maarifa ambayo yatachangia kuleta mabadiliko katika Taaluma ya Uhandisi.
Wiki ya 12 ya Uhandisi wa Afrika ya UNESCO unaofanyika sambamba na Mkutano wa Kumi (10) wa Uhandisi wa Afrika 2026 umejumuisha washiriki kutoka nchi 29 za Afrika na nchi Tano kutoka nje ya Bara la Afrika.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amaekagua mabanda ya maonesho na kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na wahandisi wa ndani na nje ya nchi.