MWENYEKITI WA CCM MKOA WA RUVUMA ODDO MWISHO WANACHAMA CCM LIPENI ADA ILI KUIMAIRISHA CHAMA
KAHAWA DIGITAL TV
0:00 / 0:00
MWENYEKITI WA CCM MKOA WA RUVUMA ODDO MWISHO WANACHAMA CCM LIPENI ADA ILI KUIMAIRISHA CHAMA
130 просмотров · 12 дней назад
KAHAWA DIGITAL TV
605 подписчиков
130 просмотров · 12 дней назад
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, ODDO MWISHO, ameanza ziara ya kuimarisha chama katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma, ikiwa na lengo la kutoa shukrani kwa wananchi na wanachama kwa kuendelea kukiamini chama hicho.
Katika ziara hiyo, Mwenyekiti huyo anatarajiwa kukutana na viongozi na wanachama wa CCM kuanzia ngazi ya shina Hadi wilaya huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo.
Aidha, ziara hiyo inalenga kutathmini maendeleo na uhai wa Chama Cha Mapinduzi, ikiwemo hali ya ulipaji wa ada za wanachama, suala linalotajwa kuwa muhimu katika kuimarisha shughuli na taasisi za chama.
Mwenyekiti ODDO MWISHO pia anatarajiwa kusikiliza changamoto zinazowakabili wanachama na wananchi, pamoja na kuhamasisha fursa kwa vijana kupitia mikopo na shughuli mbalimbali za kiuchumi, ili kuwawezesha kujiajiri na kukuza uchumi wao.
Ziara hiyo pia inalenga kupata picha halisi ya uhai wa chama katika maeneo mbalimbali, kuimarisha mshikamano wa wanachama na kuweka mikakati ya kukifanya chama kuwa karibu zaidi na wananchi.