Перейти к содержимому

HII HAPA TAARIFA RASMI YA JESHI LA POLISI YA KUUNGUA KWA MELI ZIWA NYASA

Baharia TV

0:00 / 0:00

HII HAPA TAARIFA RASMI YA JESHI LA POLISI YA KUUNGUA KWA MELI ZIWA NYASA

713 просмотров · 13 часов назад
Baharia TV
108 тыс. подписчиков
713 просмотров · 13 часов назад
​Watu watatu wamefariki dunia baada ya meli ya mizigo iitwayo MV Chambo, iliyosajiliwa nchini Msumbiji, kuungua moto alfajiri ya Oktoba 11, 2026, katika Ziwa Nyasa, umbali wa takribani maili 20 za Ziwa Nyasa kutoka Bandari ya Mbamba Bay, Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma. ​Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma imeeleza kuwa meli hiyo ilikuwa na abiria 44 waliokuwa wakielekea Bandari ya Mitengula nchini Msumbiji. Marehemu wametambuliwa kuwa ni Yusto Chatanda, raia wa Tanzania, Joyce Chimalilo, raia wa Malawi, na Lilian Ela Luoga, mtoto mwenye uraia wa Msumbiji. Katika ajali hiyo, abiria 41 walinusurika na kuokolewa, kisha kufikishwa katika Hospitali ya Nangombo iliyopo Wilaya ya Nyasa kwa ajili ya matibabu. ​Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hali zao zinaendelea vizuri huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika hospitali hiyo kusubiri utambuzi na uchunguzi wa daktari. ​Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na idara nyingine zinazohusika, linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo. ​Aidha, limetoa wito kwa wananchi, wavuvi na wadau wa usafiri wa majini kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji, kuhakikisha vyombo vyao vinakaguliwa na kutobeba abiria au mizigo inayozidi uwezo wake ili kuzuia ajali zinazoweza kusababisha vifo na majeraha. #BahariaNews