Перейти к содержимому

KCJE TUTASAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 KWA VYAMA VIKUU

KCJE Online

0:00 / 0:00

KCJE TUTASAMBAZA MAGUNIA MILIONI 9.3 KWA VYAMA VIKUU

25 просмотров · 3 нед. назад
KCJE Online
9 подписчиков
25 просмотров · 3 нед. назад
Meneja Mkuu wa Korosho Cooperative Joint Enterprise (KCJE) Limited, Mohamed Mwinguku, amesema KCJE imejipanga kuhakikisha hakutakuwa na changamoto ya upatikanaji wa magunia katika msimu wa korosho wa 2026/2027. Mwinguku amesema makadirio ya uzalishaji wa korosho kwa msimu huo ni tani 750,000, huku mahitaji ya magunia yakikadiriwa kufikia zaidi ya milioni 9.35. “Kwa msimu wa 2026/2027 tumejipanga vizuri kuhakikisha changamoto za magunia hazijitokezi. Makadirio ya uzalishaji ni tani 750,000, huku mahitaji ya magunia yakikadiriwa kuwa zaidi ya milioni 9.35,” amesema. Amesema hadi sasa, jumla ya magunia milioni 13 yamehifadhiwa katika maghala, hali ambayo inaonyesha kuwa kuna akiba ya kutosha kukidhi mahitaji ya msimu huo. “Hii ina maana kwamba, ukilinganisha na mahitaji ya magunia milioni 9.35, tuna ziada ya zaidi ya magunia milioni 3.5,” amefafanua. Kwa mujibu wa Mwinguku, uwepo wa akiba hiyo unatarajiwa kusaidia kuzuia changamoto za upatikanaji wa magunia katika maghala, vituo vya usafirishaji na maeneo mengine ya mnyororo wa usambazaji wakati wa msimu wa korosho. Aidha, amesema mifumo ya mizani ya kidijitali imekamilika na ipo tayari kutumika, huku watendaji pamoja na wadau wengine wanaohusika katika mchakato wa ukusanyaji na uuzaji wa korosho wakiwa wamejipanga kuanza kazi. Mwinguku amesema maandalizi hayo yanalenga kuhakikisha mchakato wa upokeaji, upimaji na usafirishaji wa korosho unafanyika kwa ufanisi katika msimu wa 2026/2027. Follow akaunti zetu za Facebook: Korosho Cooperative Instagram: Korosho Cooperative YouTube: KCJEOnline Website: www.koroshokcje.coop @ushirika_tcdc @wizara_ya_kilimo @taneculimited @lindi_mwambao_official @runaliltd_ @gmmamcultd @tamcultd @copra_tz @cashewnutboard @mcmaprosoo @wrrbwrs #KCJE #ushirikapamojatujengeuchumi