Перейти к содержимому

MZOZO WA UKUTA UPANGA: MMILIKI AITAKA SERIKALI KUIINGILIA KATI

NYAMATE DIGITAL

0:00 / 0:00

MZOZO WA UKUTA UPANGA: MMILIKI AITAKA SERIKALI KUIINGILIA KATI

83 просмотра · 3 недели назад
NYAMATE DIGITAL
1,33 тыс. подписчиков
83 просмотра · 3 недели назад
MZOZO WA UKUTA UPANGA: MMILIKI AITAKA SERIKALI KUIINGILIA KATI Mmoja wa wamiliki wa nyumba eneo la Upanga, Dar es Salaam, Bi Naida Ismail, ameiomba Serikali kuingilia kati mgogoro wa eneo hilo na jirani yake, akidai kuwa ukuta wa nyumba yake ulivunjwa nyakati za usiku bila makubaliano, hatua iliyosababisha hofu na taharuki kwa wapangaji. Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Bi Naida alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa nane usiku, ambapo watu walifika katika eneo hilo wakiwa na mashine ya kuchimba (excavator) na kuanza kubomoa ukuta. Alisema hatua hiyo ilifanyika bila makubaliano na wamiliki wa nyumba, hali iliyowafanya wapangaji kushangazwa na tukio hilo. Bi Naida alisema baada ya tukio hilo alikwenda Kituo cha Polisi Sarender kutoa taarifa, ambapo alielezwa kuwa angefika siku ya Jumatatu pamoja na jirani yake kwa ajili ya kushughulikia suala hilo. Hata hivyo, alisema kabla ya siku hiyo kufika, watu walirejea katika eneo hilo na kuendelea na ubomoaji. Mmoja wa wapangaji wa nyumba hiyo alisema tukio hilo la usiku liliwashtua na kusababisha hofu miongoni mwa wakazi wa nyumba hiyo. Alisema uharibifu uliotokea umeibua maswali kuhusu usalama wa wapangaji na mali zao, hivyo akaomba mamlaka husika kufika eneo hilo na kuchunguza suala hilo. Bi Naida ameiomba Serikali, ikiwemo uongozi wa Wilaya ya Ilala, kuingilia kati na kusaidia kutatua mgogoro huo kwa njia ya amani na kwa kuzingatia sheria. Amesema anaamini hatua hiyo itasaidia kulinda haki za pande zote na kuzuia mgogoro huo kuendelea. Kwa upande mwingine, tumejaribu kumtafuta msimamizi wa eneo hilo ili kupata majibu kuhusu tuhuma hizo na kutoa nafasi ya kueleza upande wake, lakini hakupatikana. Tunaendelea na jitihada za kumtafuta ili aweze kutoa ufafanuzi kuhusu madai yaliyotolewa na wamiliki pamoja na wapangaji wa nyumba hiyo.