Перейти к содержимому

UMEKOSA NINI WE YESU LYRICS | KWARESMA | LENT SONG | FULL MEDIA

Full Media

0:00 / 0:00

UMEKOSA NINI WE YESU LYRICS | KWARESMA | LENT SONG | FULL MEDIA

4 367 просмотров · 1 год назад
Full Media
3,29 тыс. подписчиков
4 367 просмотров · 1 год назад
Umekosa Nini we Yesu, kushtakiwa bure kwa Pilato Wenye kustahili hukumu, si wewe, si wewe, Bwana ni sisi Ole msalaba huo mzito, apagazwa Mwana Mpenzi wa Mungu Mwili waenea mateso, alipa, alipa madhambi yetu Ona Mumba Mbingu na nchi, yupo chini mzigo wamwelemea Na mtu kiumbe chake kwa ukali, ampiga, ampiga bila huruma Huko njiani we Maria, waonaje hali ya mwanao Ni damu tupu na vidonda, machozi, machozi yamfumba macho Kwa Simoni heri ya kweli, mimi pia Yesu nisaidie Kuchukua mzigo wa ukombozi, kuteswa, kuteswa pamoja nawe Uso wa Yesu malaika, Bethlehemu wakuabudu Bahati yake Veronika, kupangusa, kupangusa mfalme wa mbingu Wakimvuta huku na huku, wauaji wakamchokesha bure Chini wamtupa bado kwa nguvu, aibu, aibu yao milele Wanawake wa Israeli, msilie kwa sababu hiyo Muwalilie hao kwa dhambi, upanga, upanga ni juu yao Mwokozi sasa ni ya tatu, kuanguka chini ya msalaba Katika dhambi za ulegevu, nijue, nijue kutubu hima Muje malaika wa Mbingu, funikeni mwiliwe kwa huruma Vidonda vyake na utupu, askari, askari wamvulia Hapo mkristu ushike moyo, Bwana wako alazwa msalabani Mara miguu na mikono, yafungwa, yafungwa kwa misumari Yesu mpenzi nakuabudu, msalabani unapohangaika Nchi yatetemeka kwa hofu, na jua, na jua linafifia Mama Maria mtakatifu, upokee maiti ya mwanao Tumemwua kwa dhambi zetu, twatubu, twatubu kwake na kwako Pamoja naye kaburini, zika dhambi na ubaya wa moyo Yesu tuwe wakristu wa kweli, twakupa, twakupa sasa mapendo * * * * * * * * Katika roho yangu Bwana, chora mateso niliyokutesa Nisiyasahau madeni, na kazi, na kazi ya kuokoa