Перейти к содержимому

KILIO KIMESIKIKA, KINA CHA MTO MBEZA CHACHIMBWA, NI TAHADHARI YA EL NINO SASA!

AMASHI TV

0:00 / 0:00

KILIO KIMESIKIKA, KINA CHA MTO MBEZA CHACHIMBWA, NI TAHADHARI YA EL NINO SASA!

5 просмотров · 4 часа назад
AMASHI TV
7,19 тыс. подписчиков
5 просмотров · 4 часа назад
Ni Zaidi Ya Miezi Mitano Sasa Imepita Tangu Mafuriko Makubwa Yalipoleta Madhara Kwa Wakazi Wa Mji Wa Korogwe Hususani Katika Soko La Manundu. Kwa Mujibu Wa Mbunge Wa Korogwe Mjini Cpa Charles Mhando Njama Wafanyabiashara Wa Soko Hilo Walipata Hasara Ya Takribani Bilioni 1.7, Wakati Huo, Ahadi Za Kutafuta Suluhisho Zilitolewa. Leo Tumerejea Kwenye Kiini Cha Tatizo Kujua, Je Kuna Hatua Zimeanza Kuchukuliwa? Na Hapa Ni Mto Mbeza, Ambapo Kujaa Kwa Kina Chake Kumelalamikiwa Kuwa Chanzo Cha Mafuriko Yaliyotokea Miezi Michache Iliyopita, Mvua Ya El Nino Inayotarajiwa Kunyesha Oktoba Mwaka Huu, Inaonekana Kuchochea Tahadhari Zaidi Kwa Wakazi Wa Mji Wa Korogwe Na Leo Jibu Linaonekana Kuanza Kujitokeza Kupitia Kauli Ya Mbunge Wa Korogwe Mjin Cpa Charles Mhando Njama Aliyoitoa Kwenye Mkutano Wake Wa Hadhara Na Wananchi Wa Kata Ya Manundu Uliofanyika Septemba 18,2026 Katika Viwanja Vya Ofisi Ya Kata Ya Manundu Mjini Korogwe. Tumefika Mto Mbeza Na Kushuhudia Mtambo Wa Excavator Ukiendelea Na Kazi Ya Kurejesha Kina Cha Mto. Hatua Hii Inalenga Kuongeza Uwezo Wa Maji Kupita Kwenye Njia Yake Hasa Wakati Wa Mvua Kubwa, Na Kupunguza Hatari Ya Maji Kujaa Na Kuelekea Kwenye Maeneo Ya Watu. Juhudi Hizi Zitaleta Matokea Chanya Kwa Muda Mrefu Endapo Wananchi Watakuwa Mstari Wa Mbele Kutunza Mazingira Na Kudumisha Usafi Wa Maeneo Yao, Pamoja Na Mamlaka Husika Kutimiza Wajibu Wake Kwa Wakati Katika Kuzoa Taka. Lakini Swali Kubwa Linabaki, Je, Kazi Hizi Zitaweza Kupunguza Madhara Pale Mvua Kubwa Zitakaponyesha? Jibu Lake Halipatikani Kwenye Maneno Pekee, Bali Katika Hali Ya Manundu Wakati Wa Mvua Kubwa Zitakaponyesha Tena. Ni Kongole Kwa Viongozi Kueleza Na Kuonesha Hatua Zinazochukuliwa Katika Kutafuta Suluhisho, Na Wananchi Kukumbushwa Wajibu Wao Wa Kulinda Mazingira Na Kuimarisha Usafi.