TANZANIA YAWASILISHA MAGEUZI NA MAFANIKIO YA HAKI ZA BINADAMU KATIKA JUKWAA LA UMOJA WA MATAIFA
Katiba na Sheria Channel
0:00 / 0:00
TANZANIA YAWASILISHA MAGEUZI NA MAFANIKIO YA HAKI ZA BINADAMU KATIKA JUKWAA LA UMOJA WA MATAIFA
12 просмотров · 14 ч назад
Katiba na Sheria Channel
317 подписчиков
12 просмотров · 14 ч назад
Tanzania imewasilisha mafanikio na hatua mbalimbali ilizochukua katika kuimarisha ulinzi na utekelezaji wa haki za binadamu, ikieleza mageuzi yaliyofanyika katika sekta ya sheria na haki, demokrasia, utawala bora, usawa wa kijinsia pamoja na upatikanaji wa huduma za kijamii, katika Kikao cha Nne cha Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu kwa Mataifa (Universal Periodic Review – UPR) kinachofanyika katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi.
Katika wasilisho hilo lililofanyika Novemba 5, 2026, Tanzania imeeleza hatua zilizotekelezwa katika kipindi cha tathmini, ikisisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha taasisi, mifumo ya utoaji haki na kulinda utu wa kila mtu kwa kuzingatia Katiba, sheria za nchi na wajibu wa kimataifa wa haki za binadamu.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa katika tathmini iliyopita mwaka 2021, Tanzania ilipokea jumla ya mapendekezo 252 kutoka kwa nchi mbalimbali, ambapo ilikubali mapendekezo 187, yakiwemo 20 yaliyokubaliwa kwa sehemu, huku mapendekezo 65 hayakukubaliwa. Mapendekezo yaliyokubaliwa yamekuwa sehemu ya msingi wa mageuzi na hatua zilizotekelezwa katika kipindi cha taarifa.