Перейти к содержимому

ULEGA ATILIA MKAZO MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO

Katiba na Sheria Channel

0:00 / 0:00

ULEGA ATILIA MKAZO MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO

71 просмотр · 3 нед. назад
Katiba na Sheria Channel
317 подписчиков
71 просмотр · 3 нед. назад
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdallah Hamis Ulega, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto kupitia ushirikiano wa taasisi za Serikali na wadau mbalimbali, ili kuhakikisha watoto wanalindwa na kupata haki stahiki. Mhe. Ulega ameyasema hayo tarehe 13 Oktoba, 2026 katika ziara yake ya kujitambulisha ambapo amekutana na Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo Njedengwa, jijini Dodoma. Katika ziara hiyo Waziri Ulega amepokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo na kujadili mipango ya kuimarisha huduma za kimashtaka nchini. Amesema ni muhimu kuimarisha juhudi za kuanzisha kituo maalumu cha kushughulikia mashauri ya ukatili dhidi ya watoto, akieleza kuwa hatua hiyo inahitaji ushirikiano wa karibu kati ya Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na wadau wengine.