Перейти к содержимому

AANGUA KILIO AKIKUMBUKA BABU DUNI ALIVYOJIONDOA KUGOMBEA UWENYEKITI ACT WAZALENDO

Mwananchi Digital

0:00 / 0:00

AANGUA KILIO AKIKUMBUKA BABU DUNI ALIVYOJIONDOA KUGOMBEA UWENYEKITI ACT WAZALENDO

5 008 просмотров · 2 г. назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
5 008 просмотров · 2 г. назад
Mjumbe wa Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo, Ally Salehe, ameshindwa kujizuia na kumwaga machozi wakati akielezea jinsi mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Juma Duni Haji, alivyojitoa katika mbio za kusaka uenyekiti. Salehe amesimulia kuwa, Babu Duni alijitoa siku tano kabla ya uchaguzi ili kumpisha Othman Masoud Othman na alifanya hivyo kwa lengo la kulinda umoja na uimara wa chama. “Tulipomuuliza kwa nini asijitoe jina lake mapema, alisema kwanza alitaka autumikie uenyekiti wake mpaka mwisho, pili alisema wacha chama kijenge uzoefu wa mitikisiko ili kijenge uimara wake, tumevuka na tunajiandaa kwa ushiriki na ushindi hapo mwakani,” amesema Salehe. Huku akibubujikwa na machozi ameposema: "Babu Duni ni muumini wa taasisi imara." Sherehe ya kumuenzi Babu Duni kwa mchango wake katika chama imefanyika leo Jumatano Septemba 4, 2024 Kiembe Samaki, Zanzibar. (Imeandikwa na Faraja Masinde)