UMEWAHI KUFIKA KATIKA MNARA WA MAAJABU - KINUMOSHI
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
UMEWAHI KUFIKA KATIKA MNARA WA MAAJABU - KINUMOSHI
360 просмотров · 15 часов назад
ASAM Online TV
22,3 тыс. подписчиков
360 просмотров · 15 часов назад
Ushirika wa Mwanamke Mpambanaji umeandaa ziara maalum kwa watembeza wageni kutembelea na kufahamu zaidi Kinumoshi Magic Tower and Spice Farm, eneo lililopo Kizimbani, Wilaya ya Magharibi A Unguja, linalojumuisha vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo mnara wa kimajabu na shamba la viungo.
Ziara hiyo imelenga kuwapa watembeza wageni fursa ya kufahamu historia, mazingira na vivutio vilivyopo katika eneo hilo, ili nao waweze kuvitambulisha kwa watalii wanaofika Zanzibar.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa Kinumoshi Magic Tower and Spice Farm, Rehema Shaaban Jabu, amesema lengo ni kulitambulisha eneo hilo kwa watembeza wageni na kuwapa uelewa mpana kuhusu historia pamoja na vivutio vilivyopo, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii wanaolitembelea.
Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa ziara hiyo wamesema wamevutiwa na kushangazwa na historia ya eneo hilo, wakieleza kuwa Kinumoshi Magic Tower and Spice Farm ina vivutio mbalimbali vinavyoweza kuwa sehemu muhimu ya utalii wa Zanzibar.
Ziara hiyo imekuwa pia fursa ya kuwakutanisha wadau wa utalii na kuendelea kutafuta namna bora ya kutangaza vivutio vya Zanzibar ambavyo bado havijafahamika kwa kiwango kikubwa.
#AsamOnlineTV #ZanzibarNews #UtaliiZanzibar #Kizimbani #Kinumoshi #SpiceFarm #TourismZanzibar #ZanzibarTourism #HabariZanzibar #TravelZanzibar #NewsUpdate #Trending