UNAPATA CHOO KWA SHIDA (constipation)? SABABU NA NJIA ZA KUTATUA TATIZO HILI
Dr. Faraja M.
0:00 / 0:00
UNAPATA CHOO KWA SHIDA (constipation)? SABABU NA NJIA ZA KUTATUA TATIZO HILI
68 просмотров · 20 ч назад
Dr. Faraja M.
2,07 тыс. подписчиков
68 просмотров · 20 ч назад
Je, unapata choo kwa shida? Unakaa siku kadhaa bila kupata choo, choo kinakuwa kigumu, au unalazimika kutumia nguvu nyingi unapojisaidia?
Tatizo hili linajulikana kama CONSTIPATION au kufunga choo. Linaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye nyuzinyuzi chache, kutokunywa maji ya kutosha, kutofanya mazoezi, baadhi ya dawa na matatizo mengine ya kiafya.
Katika video hii, Dkt. Faraja anaeleza:
✅ Constipation ni nini na dalili zake.
✅ Sababu kuu za kupata choo kigumu.
✅ Vyakula vinavyoweza kusaidia kurahisisha upatikanaji wa choo.
✅ Umuhimu wa maji, mazoezi na tabia nzuri za kujisaidia.
✅ Ni wakati gani unapaswa kutumia dawa na lini unapaswa kumuona daktari.
✅ Dalili za hatari ambazo hazipaswi kupuuzwa.
Lengo ni kukusaidia kuelewa tatizo la constipation na kujua hatua zinazoweza kusaidia kuboresha afya yako ya mfumo wa chakula.
📌 Kama video hii imekusaidia, LIKE, SHARE na SUBSCRIBE kwenye channel hii kwa elimu zaidi kuhusu afya ya mfumo wa chakula, saratani, afya ya wanaume, wanawake na watoto.
💬 SWALI: Je, umewahi kupata tatizo la choo kigumu? Ni jambo gani limekuwa likikusaidia? Tuandikie kwenye sehemu ya maoni.
#Constipation #ChooKigumu #AfyaYaMfumoWaChakula #Afya #DrFaraja