Перейти к содержимому

#TBCDIGITAL : AJALI YA BUS LA ISAMILO NA LIBANIKA VIFO TISA | MASHUHUDA WA AJALI WASIMULIA

TBConline

0:00 / 0:00

#TBCDIGITAL : AJALI YA BUS LA ISAMILO NA LIBANIKA VIFO TISA | MASHUHUDA WA AJALI WASIMULIA

23 128 просмотров · 3 мес. назад
TBConline
532 тыс. подписчиков
23 128 просмотров · 3 мес. назад
Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria eneo la Ibihwa, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, imeongezeka na kufikia tisa, huku uchunguzi wa awali ukibaini kuwa chanzo chake ni uzembe wa dereva wa basi la Kampuni ya Isamilo ambaye tayari amekamatwa. Ajali hiyo ilihusisha basi la Kampuni ya Isamilo lililokuwa likitoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam na basi la Libanika Luxury lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari jioni ya leo, Agosti 2, 2026, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Asifiwe Ulime, amesema miili miwili tayari imetambuliwa na ndugu zao. Amewataja waliotambuliwa kuwa ni Hassan Issa na Casto Kibwana, huku miili mingine ikiendelea kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na Kituo cha Afya cha Makole kusubiri kutambuliwa na ndugu