Перейти к содержимому

TONE LA KWANZA LA MAFUTA MRADI WA EACOP KUONEKANA FEBRUARI 2027

SILILU MEDIATV

0:00 / 0:00

TONE LA KWANZA LA MAFUTA MRADI WA EACOP KUONEKANA FEBRUARI 2027

4 300 просмотров · 4 недели назад
SILILU MEDIATV
497 подписчиков
4 300 просмотров · 4 недели назад
Serikali imesema kufikia mwezi Desemba mwaka huu, vituo vyote vya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki –EACOP- kwa nchi za Uganda na Tanzania, vitakuwa vimekamilika kwa ajili ya kuanza kupitisha mafuta. Mradi huo una urefu wa kilomita 1,443, kati ya hizo kilomita 296 zipo upande wa nchi ya Uganda na kilomita 1,147 zipo Tanzania. Akizungumza wakati alipotembelea kutuo namba tatu cha kusukuma Mafuta Ghafi, kilichoko katika kijiji cha Kikagate kata Mubunda wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji kutoka shirika la Maendeleo la Mafuta Tanzania – TPDC, Derick Moshi kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa TPDC, amesema inategemewa tone la kwanza la mafuta litaanza kuonekana Februari mwaka 2027. Naye mwakilishi wa mradi wa EACOP katika kituo cha kusukuma Mafuta Ghafi namba tatu, Dmitry Malyshev amesema kuwa hatua ya utekelezaji wa mradi huo katika kituo hicho ni zaidi ya asilimia 90, na kwamba wanatarajia kufikia mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, utakamilika. Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki, kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga Tanzania, una umiliki wa Taasisi nne ambazo ni TPDC ya Tanzania asilimia 15, UNOC ya Uganda asilimia 15, Total Energy ya Ufaransa asilimia 62 na SNOOC ya nchini China asilimia nane.    • TONE LA KWANZA LA MAFUTA MRADI WA EACOP KU...