WWANANCHI WAFUNGUKA, WATOA KERO ZAO KWENYE KAMPENI YA “ONGEA NA KAMANDA"
Baharia TV
0:00 / 0:00
WWANANCHI WAFUNGUKA, WATOA KERO ZAO KWENYE KAMPENI YA “ONGEA NA KAMANDA"
59 просмотров · 1 дн. назад
Baharia TV
108 тыс. подписчиков
59 просмотров · 1 дн. назад
Wananchi wa eneo la Lukobe Senta, Kata ya Lukobe, Manispaa ya Morogoro, wamepata fursa ya kueleza maoni, ushauri na kero mbalimbali zinazohusu usalama na utendaji wa Jeshi la Polisi, mbele ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, Oktoba 6, 2026, katika muendelezo wa Kampeni ya “Ongea na Kamanda.”
Miongoni mwa kero zilizowasilishwa na wananchi ni pamoja na kuanzishwa kwa operesheni dhidi ya watu wanaohusika na biashara na usambazaji wa dawa za kulevya pamoja na wakulima wanaojihusisha na kilimo hicho.
Aidha, wananchi waliomba kuimarishwa kwa usimamizi wa maadili na mienendo ya watoto pamoja na kupewa elimu zaidi kuhusu namna ya kujikinga na uhalifu.
Akizungumza katika kampeni hiyo, ACP Kantimbo amesema Kampeni ya “Ongea na Kamanda” imelenga kuifikia jamii moja kwa moja, kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na kuweka mikakati ya pamoja ya kuzuia uhalifu kuanzia ngazi ya familia hadi jamii kwa ujumla.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wamepongeza hatua ya Jeshi la Polisi kuwapa nafasi ya kueleza kero na kutoa ushauri, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uhalifu na viashiria vya uhalifu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
#BahariaNews