Перейти к содержимому

WATOTO ZAIDI YA 300 NZIHI WAHITAJI MABORESHO UPATIKANAJI HUDYMA YA MALEZI MCHANA

Makutano TV

0:00 / 0:00

WATOTO ZAIDI YA 300 NZIHI WAHITAJI MABORESHO UPATIKANAJI HUDYMA YA MALEZI MCHANA

113 просмотров · 2 месяца назад
Makutano TV
4,2 тыс. подписчиков
113 просмотров · 2 месяца назад
Mradi wa Kituo cha Malezi ni mpango wa maendeleo ya mtoto (ECD) unaolenga kuboresha upatikanaji wa huduma salama, jumuishi, na zinazoendeshwa na jamii kwa watoto wadogo nchini Tanzania. Mradi huu unalenga katika kusaidia jamii kuanzisha na kusimamia Vituo vya Kulelea Watoto kwa Msingi wa Jamii (CBDCs) ambavyo vinakuza ukuaji kamili, kujifunza na ulinzi kwa watoto katika miaka yao ya mapema. Timu ya utekelezaji PJT-MMMAM Mkoa wa Iringa imefika hapa Iringa Vijijini Kijiji cha Nzihi kwa hatua za kubaini mahitaji ya uwepo wa vituo vya malezi ya watoto mchana. IDYDC inatekeleza mradi huu kama sehemu ya juhudi za kitaifa zinazoratibiwa na Mtandao wa Maendeleo ya Awali Tanzania (TECDEN), kwa ufadhili wa Echidna Giving. Mradi huu unachangia moja kwa moja katika vipaumbele vya kitaifa kuhusu Maendeleo ya Awali ya Mtoto na ustawi wa mtoto. Project Goal Kuboresha upatikanaji wa huduma bora, jumuishi na za maendeleo zinazoongozwa na jamii kwa watoto wenye umri wa miaka 2-5, na kuwezesha familia na jamii kusaidia ukuaji wa watoto. Kwa mujibu wa Serikali ya Kijiji , Kijiji cha Nzihi kina vitongoji 8 na kati ya hivyo 4 viko pembezoni na Kijiji kinakadiliwa kuwa na watoto wenye umri chini ya miaka 5 wapatao 300 ambao wanahitaji kupatiwa huduma katika vituo vya malezi.