Перейти к содержимому

UWEKEZAJI WA RASLIMALI FEDHA KATIKA HALMASHAURI UTEKELEZAJI PJT MMMAM 2026

Makutano TV

0:00 / 0:00

UWEKEZAJI WA RASLIMALI FEDHA KATIKA HALMASHAURI UTEKELEZAJI PJT MMMAM 2026

139 просмотров · 1 месяц назад
Makutano TV
4,21 тыс. подписчиков
139 просмотров · 1 месяц назад
Kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Sura 290 inaipa mamlaka Halmashauri hapa Nchini kupanga, kusimamia, na hukusanya fedha kupitia ushuru wa masoko, leseni za biashara, na vyanzo vingine vya ndani, swali ni Je, mtoto wa Kitanzania anapata fungu gani katika keki hii ya kiuchumi? Kwa miaka mingi, asilimia kubwa ya mapato ya ndani imekuwa ikielekezwa kwenye miredi kuimarisha mawe na saruji, huku rasilimali watu ya kesho—ambayo ni watoto—ikibaki hatarini. Matukio ya ukatili, ukosefu wa lishe bora, na uhaba wa vituo salama vya kulelea watoto vingali changamoto sugu. Leo tupo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa tukiangazia uwekezaji wa Raslimali fedha kwa watoto chini ya Miaka 5 kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya afua za mtoto. Naanza kwa kuzungumza na Afisa anayetajwa na Mkurugenzi kuwa ni Kinara wa Lishe Anzael Msigwa Afua za mtoto si hisani, ni uwekezaji wa kimkakati. Wataalamu wa maendeleo wanasisitiza kuwa, kutenga bajeti thabiti kutoka kwenye mapato ya ndani kwenda kwenye sekta ya ustawi wa jamii ndiyo ngao pekee ya kulinda haki za mtoto. Fedha hizi zinahitajika kugharamia mifumo ya ulinzi, ununuzi wa virutubisho vya lishe, kuboresha madarasa ya elimu ya awali, na kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, HAPA Halmashauri ya Manispaa mkakati wa uwekezaji upoje? Sheria ya Mtoto Kifungu cha 10 kinalazimisha Serikali za Mitaa (Halmashauri) kutenga rasilimali za kutosha kulinda haki za watoto, kuendesha mabaraza ya watoto, na kutunza madaftari ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, kwa sasa nazungumza na Mkurugenzi Bi Zaina Mlawa anasema na timu yake wamejidhatiti katika kipaumbele cha mtoto Ujenzi wa taifa imara unaanza na uwekezaji kwa mtoto wa leo. Ni wakati sasa kwa mabaraza ya madiwani na wapanga mipango wa halmashauri kuwapa watoto kipaumbele wanachostahili kwenye meza ya ugawaji wa mapato. Mkurugenzi Mlawa ameonyehsa mfano huu wa uthubutu na wa kuigwa kwa utengaji na utolewaji wa fedha za mapato ya ndani kwa uwekezaji wa mtoto na kwa asilimia 97 kwa afua ya Lishe, Si hivyo tu na sasa ameibeba ajenda ya watoto wwenye mahitaji maalum mabegani kuhakikisha wanapata haki ya elimu na ulinzi na usalama wao. END