MHE HEMED AFUNGUKA PEMBA! SERIKALI YAPIGA HATUA KUBWA KILIMO NA KUIMARISHA UZALISHAJI WA CHAKULA!
Tifu Tv
0:00 / 0:00
MHE HEMED AFUNGUKA PEMBA! SERIKALI YAPIGA HATUA KUBWA KILIMO NA KUIMARISHA UZALISHAJI WA CHAKULA!
226 просмотров · 1 дн. назад
Tifu Tv
44,8 тыс. подписчиков
226 просмотров · 1 дн. назад
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yanaendelea kuwa Jukwaa muhimu la kuibua, kuonesha na kukuza fursa zilizopo katika Sekta ya Kilimo na Ufugaji.
Ameyasema hayo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya CHAMANANGWE Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Amesema Maonesho hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza uelewa kwa wakulima na wafugaji, kuhamasisha matumizi ya Teknolojia na mbinu bora za kilimo na ufagaji, kuongeza tija ya uzalishaji kwa kuwaunganisha wakulima, wafanyabiashara, wataalamu, wawekezaji na wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo na ufugaji.
Mhe. Hemed amefahamisha kuwa Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2050 imeeleza muelekeo wa Kimkakati katika Sekta ya Kilimo ni kukibadilisha kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo endelevu cha biashara kinachostahmili mabadiliko ya hali ya hewa na kuongeza thamani kwa utoshelevu wa chakula na mauzo ya ndani na nje ya nchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema kwa lengo la kufikia dhamira hio, Serikali ya Awamu ya Nane imefanya juhudi mbali mbali ikiwemo kuifanyia matengenezo miundombinu ya umwagiliaji katika mabonde kumi (10) ya mpunga Unguja na Pemba, ujenzi wa Maghala ya kuhifadhia mbegu pamoja na kuyafanyia ukarabati Maghala ya kuhifadhia chakula.
Mhe. Hmed amesema kuwa Serikali inaendelea kuharakisha Mpango wa Mageuzi ya Sekta ya Kilimo Zanzibar (2025-2035) ili uweze kuwanufaisha wananchi kwa kuongeza tija katika shughuli zao za uzalishaji na kuongeza kipato.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na wataalamu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) pamoja na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar juu ya uwepo wa Mvua kubwa za Vuli ambazo zianatarajiwa kunyesha mwezi huu zitakazo ambatana na EL NINO ili waweze kuchukua tahadhari ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza.
Aidha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wananchi kusafisha mitaro ya maji ya mvua, kuhama katika maeneo hatarishi kama vile, mabondeni na kwenye vyanzo vya maji sambamba na kuacha tabia ya kutupa taka ovyo ili kudhibiti maradhi yanayosababishwa na uchafu ikiwemo kipindu pindu.
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. SULEIMAN MASSOUD MAKAME amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kutumia mifumo ya Kisayansi katika kutekeleza ukulima na ufugaji wa kisasa wenye tija na jumuishi wenye kustahmili mabadiliko ya Tabia nchi.
Mhe. Makame amesema Wizara inaendelea kufanya tafiti mbalimbali ili kuhakikisha Sekta ya Kilimo inakuwa na kuimarika hasa katika matumizi ya Teknolojia, upanuzi wa masoko na kulima kilimo chenye tija ambacho kitatoa uhakika wa upatikanaji wa chakula cha kutosha nchini.
Mhe. Massoud amewataka wakulima na wafugaji kuendeleza ushirikiana na Taasisi mbali mbali zinazoshiriki katika maonesho hayo ili kuweza kubadilishana uzoefu, kupeana maarifa tatakayosaidia kuboresha zaidi maonesho hayo na kazi zinazofanywa na wakulima na wafugaji.
Akisoma taarifa ya kitaalamu kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Afisa mdhamini wa Wizara hio Mhandisi IDRISA HASSAN ABDALLA amesema Wizara ya Kilimo inaendelea na jitihada za kuhakikisha wakulima na wafugaji wanaondokana na kilimo cha mazoea na kujikita katika kilimo cha biashara kilimo endelevu chenye tija kwa faida ya wakulima, wafugaji na Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwepo kwa maonesho ya siku ya chakula dunia ni fursa kwa wakulima na wafugaji kujifunza na kutambua mbinu bora za kisasa ambazo watazitumia katika shughuli zao za kilimo na ufugaji.
Amesema zaidi ya shilingi Milioni 77 zimetumika kuboresha miundombinu mbalimbali katika maeneo ya maonesho ili kuwawezesha wakulima, wafugaji na Taasisi zaidi ya 130 zimeshiriki katika maonesho hayo ambazo zitapata fursa ya kuonesha, kutangaza na kuuza bidhaa zao.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametembelea, vitalu vya wakulima pamoja na mabanda ya maonesho kwa lengo la kujionea kazi mbali mbali zinazofanywa na wakulima, wafugaji na wadau wa Sekta ya Kilimo.