Перейти к содержимому

KOROSHO TANI 112,303 ZENYE THAMANI YA BILIONI 368.57 ZAUZWA KATIKA WIKI MBILI ZA MINADA

KCJE Online

0:00 / 0:00

KOROSHO TANI 112,303 ZENYE THAMANI YA BILIONI 368.57 ZAUZWA KATIKA WIKI MBILI ZA MINADA

182 просмотра · 10 дн. назад
KCJE Online
9 подписчиков
182 просмотра · 10 дн. назад
Jumla ya tani 112,303 za korosho ghafi zimeuzwa kwa thamani ya Sh368.57 bilioni katika minada 10 iliyofanyika katika wiki mbili za mwanzo za msimu wa mauzo wa korosho wa 2026/2027. Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred, amesema mwenendo wa soko umeendelea kuwa mzuri, huku akivipongeza vyama vikuu vya ushirika kwa juhudi za kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao kwa wakati. Alfred amesema bei ya juu iliyopatikana hadi sasa ni Sh 3,430 kwa kilo, huku bei ya chini ikiwa Sh 2,970 kwa kilo kwa korosho daraja la kwanza. Ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya korosho zilizouzwa katika kipindi hicho zilikuwa daraja la kwanza, hali inayoonyesha juhudi zinazofanywa na wakulima na wadau wengine katika kusimamia ubora wa zao hilo.