Перейти к содержимому

CCM YAITANGULIA ACT KUTOA PONGEZI KWA OMO

ZANZIBAR YETU

0:00 / 0:00

CCM YAITANGULIA ACT KUTOA PONGEZI KWA OMO

3 347 просмотров · 1 день назад
ZANZIBAR YETU
10,5 тыс. подписчиков
3 347 просмотров · 1 день назад
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis amempongeza Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi kwa kumteuwa Othman Masoud Othman kuwa malamunwa kwanza wa Rais. Mbeto ameyasema hayo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kutangaza jina la Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia vyombo vya habari. Amesema uteuzi wa Othman Masoud Othman unalenga kuendeleza umoja na mshikamano wa kisiasa, huku akieleza matarajio ya CCM kuwa viongozi walioteuliwa watatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Katiba na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo chama hicho kilishinda katika uchaguzi wa mwaka 2025. Mbeto amesema Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekamilika kwa upande wa muundo na utendaji, hivyo CCM itaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali, Rais, Makamu wa Kwanza wa Rais, Makamu wa Pili wa Rais pamoja na mawaziri, ili kutekeleza majukumu yao ya kuwaletea wananchi maendeleo. Amesema ni vyema kwa wafuasi wa vyama vya siasa kutumia kauli zinazohimiza umoja, mshikamano na maendeleo ya wananchi, badala ya kutumia lugha ya vijembe, kejeli au matusi dhidi ya viongozi. Akizungumzia nafasi ya vyama vya siasa, Mbeto amesema kila chama kitaendelea kusimamia misingi na itikadi zake, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia umoja na mshikamano kwa ajili ya kuimarisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Amesema umoja huo ni muhimu katika kuhakikisha Serikali inakuwa imara na inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar.