Перейти к содержимому

POLISI KARAGWE YATOA ONYO KWA MAAFISA USAFIRISHAJI (BODABODA)

H MEDIA

0:00 / 0:00

POLISI KARAGWE YATOA ONYO KWA MAAFISA USAFIRISHAJI (BODABODA)

5 035 просмотров · 11 дн. назад
H MEDIA
1,25 тыс. подписчиков
5 035 просмотров · 11 дн. назад
POLISI KARAGWE YATOA ONYO KWA MAAFISA USAFIRISHAJI, YAWATAKA KUPUNGUZA MWENDO KASI Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, SSP Abdalah Shaban Nyandular, amewataka maafisa usafirishaji wilayani humo kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, ikiwemo kupunguza mwendo kasi na kuhakikisha wanamiliki leseni halali za udereva. Nyandular ametoa rai hiyo Oktoba 21, 2026, wakati akizungumza na maafisa usafirishaji wanaofanyia shughuli zao Kwa kupaki Katika kituo cha Ruge Stationery mjini Kayanga, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuzingatia taratibu za usalama ili kulinda maisha yao na watumiaji wengine wa barabara. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa maafisa usafirishaji kituoni hapo, Katunzi Abdu, amelishukuru Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Usalama Barabarani kwa kutoa elimu, huku akiwataka madereva kutumia vyombo vyao vya moto kwa uangalifu, kuwa na lugha nzuri kwa wateja, kudumisha usafi wanapokuwa kazini na kupunguza safari za usiku. Abdu pia amesisitiza umuhimu wa kupunguza mwendo kasi katika maeneo yenye msongamano wa watu ili kuepusha ajali na kuimarisha usalama barabarani.