Uzinduzi Mkubwa Ligi ya Polisi Jamii Cup 2026 Karagwe
H MEDIA
0:00 / 0:00
Uzinduzi Mkubwa Ligi ya Polisi Jamii Cup 2026 Karagwe
173 просмотра · 1 мес. назад
H MEDIA
1,25 тыс. подписчиков
173 просмотра · 1 мес. назад
POLISI JAMII CUP KARAGWE YAZINDULIWA RASMI
Mashindano ya Polisi Jamii Cup Wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera, yamezinduliwa rasmi Septemba 20, 2026 katika Uwanja wa Bashungwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, OCD wa Karagwe, SSP Abdalah Shaban Nyandular, amesema mashindano hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi kupitia michezo.
Amesema pia mashindano hayo yatahamasisha vijana kushiriki michezo, kukuza vipaji na kuwaepusha na vitendo vya kihalifu.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Karagwe, Rasul Ambay, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya, amesema mashindano hayo ni fursa ya kuimarisha uhusiano kati ya Polisi na wananchi.
Mashindano hayo yanaongozwa na kauli mbiu: “Soka Letu, Usalama Wetu Tokomeza Uhalifu Karagwe.”