BEMBEA YA MAISHA SEHEMU 4 FULL PLAY (ONYESHO I)
BOB TV ANIMATIONS
0:00 / 0:00
BEMBEA YA MAISHA SEHEMU 4 FULL PLAY (ONYESHO I)
28 654 просмотра · 2 года назад
BOB TV ANIMATIONS
15,7 тыс. подписчиков
28 654 просмотра · 2 года назад
Onyesho latokea kijijini nyumbani kwa Luka. Luka anawakaribisha rafikize, Beni na Yona kwa sherehe ya kufurahia mazao yake. Beni alalmikia jinsi watu waliotupa mila zao. Anahofia kwamba vizazi vijavyo havitakuwa na mila na desturi. Katika mazungumzo yao, wazee hao watatu wanakubaliana kuwa vizazi vya siku hizi vinafikiria kuwa uzungu ndio ustaarabu. Jambo hilo linatokana na malezi ya mjini ambayo mara nyingi yameachiwa wafanyakazi wa nyumbani. Wazazi wanaraukia vibaruani asubuhi na kurudi usiku watoto wakiwa wameshalala. Luka anawakumbusha wenzake kuwa mila za zamani hazikuwaruhusu watoto wa kike kwenda shuleni wala kurithi mali ila walitegemea usaidizi wa waume zao. Lakini anakubali kuwa thamani ya mtoto wa kike imepanda na nafasi yake kupanuka. Watoto wa kike wa Yona wanamulikwa katika mazungumzo haya. Japo walidharauliwa hapo awali, sasa wamekuwa nyota ya jaha. Ni wazi kwamba wao sasa ndio wanaogharamia matibabu ya mama yao katika hospitali za hali ya juu huko mjini. Hata hivyo, fikra za kitamaduni bado zinatawala. Beni anamlaumu Sara kwa kumwacha Yona peke yake akifanya kazi zote za nyumbani. Luka anapinga kauli ya Beni ya kuwadunisha watoto wa kike na mwanamke kwa jumla. Katika onyesho hili, masuala ya ulevi na athari zake, taasubi ya kiume, usawa wa kijinsia na mabadiliko yanaangaziwa.
@KatuniZaMorowa @AkiliAndMe @CNN @babybus #animation #bembeayamaisha #cartoon #kiswahilirahisi #love #bembeayamaishavideo