Перейти к содержимому

BEMBEA YA MAISHA FULL PLAY SEHEMU 2 [ONYESHO IV]

BOB TV ANIMATIONS

0:00 / 0:00

BEMBEA YA MAISHA FULL PLAY SEHEMU 2 [ONYESHO IV]

22 735 просмотров · 2 года назад
BOB TV ANIMATIONS
15,7 тыс. подписчиков
22 735 просмотров · 2 года назад
Mjini, nyumbani kwa Asna. Asna anamwandalia mamake kiamshakinywa. Mama mtu anashangaa mbona bintiye anaishi katika chumba kidogo. Bintiye anajitetea kuwa chumba hicho kiko katika mtaa wa kifahari na anakifurahia. Sara analinganisha maisha ya mjini na ya kijijini na kuona kuwa yale ya mjini yanaudhi, afadhali ya kijijini. Anasema kwamba, watu wa mjini wako mbioni kila wakati na mapato yao ni haba. Asna hakubaliani na mamake; kwake, kiwango chake cha elimu hakimruhusu kwenda kukaa kijijini. Sara anamsihi Asna aolewe amletee mjukuu. Asna hakubaliani na jambo hilo. Kulingana na Asna, ndoa ina matatizo mengi kama yale anayopitia Neema, dada yake, ambaye ingawa amesoma na kupata shahada mbili, hazimsaidii kupigana na msimamo wa kitamaduni alionao Bunju, mumewe. Badala ya kupigania mabadiliko ya msimamo wa Bunju, Neema anaonekana kuukubali kwa sababu ya uhuru wa matumizi ya mshahara wake aliopewa na Bunju. Utepetevu kazini unazungumziwa kupitia madaktari na utendakazi wao. Baadhi ya madaktari daima wako mbioni kutoka hospitali moja hadi nyingine ili kuchuma hela za ziada bila kuwazingatia wagonjwa wao kikamilifu. Masuala makuu Kuna mambo muhimu yanayojadiliwa katika onyesho hili. Jambo la kwanza ni hadhi. Ile hali ya kutaka kuishi sehemu za kifahari hata ingawa pato ni dogo. Asna anaishi maeneo ya juu ingawa mazingira ya nyumba yake ni duni. Anajikakamua kulipa kodi ya juu ya nyumba bila kujali mazingira anamoishi. Jambo la pili linaakisi athari za elimu ya juu dhidi ya mila na desturi za Kiafrika. Inasahaulika kwamba,elimu pekee bila uelewa haiwezi kubadilisha dhana na fikra za kitamaduni. Bunju ana elimu lakini elimu yake haijamtoa katika mila na desturi za jamii yake. Neema ana elimu lakini haimsaidii kuelewa chanzo cha mila na desturi za Bunju. Jambo la tatu ni kutosheka kwa mwanamke. Neema anaonekana kutosheka na hali ya mumewe ya kumruhusu kutumia pesa zake atakavyo. Hafikirii kuwa huenda ikawa ni mtego. Mara nyingi mwanamke anapopata uhuru wa aina hii, huweza kubugikwa na akili asiweze kufikiria kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadaye. Kisha mambo yanapoharibika hujikuta hana lolote la kutegemea. ‪@KatuniZaMorowa‬ ‪@FLAHO‬ ‪@cartoonnetwork‬ #tamthilia #BOBTV